Header Ads

ZIJUE SIFA ZA "MWANAUME ANAYETAKA KUWA SERIOUS NA WEWE"

Habari zenu marafiki bila shaka ni wazima wa afya
timu ya Celebrity Swaggz iko salama na inaendelea
vyema na majukumu yake leo tutaangalia jinsi
wadada watakavyo weza kumtambua mpenzi alie
na lengo la kumuoa
ATAKAYEKUOA SIFA ZAKE NI KAMA IFUATAVYO...
1. ANABADILIKA
Mwanaume Ambaye Ana Malengo Ya Kuoa
Hubadilika Kitabia.
Muda Mwingi Hutaka Kuonekana Mtu Mzima
Mwenye Sifa Nzuri.
Hatakuwa Mtu Wa Kulewa Kupita Kiasi Na
Kutapanya Mali Na
Wanawake Wengine. Tabia Zake Mbaya Za Zamani
Ataziacha
Kisa Cha Mabadiliko Hayo Kinatajwa Na
Wataalamu Wa Masuala
Ya Ndoa Kuwa Ni Pamoja Na Kumshawishi
Mwanamke
Aliyemchagua Aitikie Mwito Wa Kuwa Pamoja
Katika Maisha.
Lakini Pia Ni Kuwapa Kielelezo Chema Ndungu Au
Wazazi Wake
Wamuunge Mkono Katika Harakati Zake Za Kuoa.
2. ATAONGEZA JITIHADA ZA KUJITEGEMEA
Mara Nyingi Wanaume Walio Makini Na Tayari
Kufunga Ndoa,
Wanahitaji Kuwa Na Kipato Cha Kutosha Kuweza
Kuwahudumia
Wake Zao Na Familia Ambazo Watakuwa Nazo
Hapo Baadaye
Hivyo Wanajitahidi Kutafuta Njia Za Kupandisha
Hali Yao
Kiuchumi.
Kama Ni Muajriwa Anaweza Akaanza Kutafuta
Miradi Mingine Nje
Ya Kazi Yake Ili Imsaidie Kuongeza Kipato Cha
Kujikimu Na Hali
Ya Maisha. Kama Alikuwa Anaishi Na Wazazi
Atapanga Chumba
Na Ataanza Kujitemea.
3. ANAGUNDUA KWAMBA ANAHITAJI KUITWA BABA
Njia Nyingine Ya Kugundua Mwanaume Aliye Tayari
Kwa Ndoa Ni Pale Unapotembea Naye Barabarani,
Anawafurahia Watoto
Mnaokutana Nao Njiani Na Mara Kwa Mara
Ataonekana Kukueleza
Jinsi Atakavyowafanyia Watoto Wake Mara Baada
Ya Kuwapata
Hapo Baadaye.
Mwanaume Huyo Pia Huwa Na Tabia Ya Kufurahia
Maisha Ya
Ndoa Ya Watu Wengine Yaani Anapomuona Mke
Na Mume Wakiwa
Na Mtoto Wao Basi Hutamani Sana Mngekuwa
Nyinyi. Mnapotoka
Hukuita Mke Wake!
4. NI RAFIKI LAKINI NI MUME
KAMILI
Mwanaume Anayetaka Kuoa Anakuwa Ni Rafiki
Yako Tu Kwa
Sababu Hamjafunga Ndoa, Lakini Matendo
Anayokufanyia Hayana
Tofauti Na Yale Ya Mtu Kwa Mkewe. Kwa Mfano
Kupanga Mipango
Ya Baadaye Ya Maisha Yenu, Kukutambulisha Kwa
Ndugu Na
Rafiki Zake. Huwa Na Hamu Ya Kutaka Kujua
Matatizo Yako Na
Kukusaidia Na Wakati Mwingine Kukushirikisha
Katika Matatizo
Yanayomkabili.
Mara Nyingi Huwa Makini Sana Kutambua
Mabadiliko Ya Mapenzi
Na Hutoa Uhuru Na Kukumilikisha Vitu Vyake Kwa
Mfano Kukupa
Funguo Za Chumba Au Nyumba Yake. Hupenda
Kutoa Misaada Ya
Kumwendeleza Mpenzi Wake Kimaisha, Kama
Kumsomesha Au
Kumtafutia Kazi.
5. HUFURAHIA UKARIBU
Mwanaume Aliyetayari Kuoa Hupenda Kuwa Karibu
Na Mpenzi
Wake Na Asilimia Kubwa Ya Mazungumzo Yake
Atayaelekeza
Katika Maisha Si Ngono. Atajitoa Kusaidia Ndugu
Wa Mke Kila
Linapokuja Tatizo. Na Atalalamika Anapotengwa Na
Familia Ya
Mchumba Wake.

Kama umeipenda tunakuomba share kwa rafiki zako

No comments:

Powered by Blogger.