MWANAFUNZI CHUO CHA UALIMU KIGOMA AIBUKA MILIONEA
Mkuu wa kitengo cha Masoko na
Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Bw.Kelvin Twissa(katikati)akiongea na
Mshindi wa Droo ya mwishi ya "MAHELA "Bw.Valelian Nickodemus(22) wa Mkoa
wa Kigoma aliyejishindia shilingi Milioni 100.kushoto ni Msimamizi wa
Michezo ya kubahatisha nchini Bw.Mrisho Milau na kulia ni Meneja wa
Huduma za Ziada wa Vodacom Tanzania,Bw. Benjamin Michael.
Kutoka kushoto,Msimamizi wa
Michezo ya kubahatisha nchini Bw.Mrisho Milau,Meneja Uhusiano wa Vodacom
Tanzania Bw.Matina Nkurlu,pamoja na Meneja wa Huduma za ziada wa
kampuni hiyo, Bw. Benjamin Michael,wakichezesha droo ya mwisho ya
"MAHELA"ambapo Bw.Valelian Nickodemus(22)Mwanafunzi wa Chuo cha uwalimu
Mkoani Kigoma alijishindia kitita cha shilingi Milioni 100,kupitia
promosheni hiyo.
Mkuu wa kitengo cha Masoko na
Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Bw.Kelvin Twissa(katikati)akizungumza na
waandishi wa habari hawapo pichani mara baada ya kumpata mshindi wa
Droo ya mwishi ya "MAHELA "Bw.Valelian Nickodemus(22) wa Mkoa wa Kigoma
aliyejishindia shilingi Milioni 100.kushoto ni Msimamizi wa Michezo ya
kubahatisha nchini Bw.Mrisho Mlau na kulia ni Meneja wa Huduma za Ziada
wa Vodacom Tanzania,Bw. Benjamin Michael.
Hatimaye Mshindi wa Milioni 100 wa
Promosheni ya Vodacom Mahela amepatikana ikishuhudia Mwanafunzi chuo
cha Ualimu cha Mkoani Kigoma Bw.Valelian Nickodemus(22) akiibuka
mshindi kupitia droo kubwa iliyochezeshwa leo jumatatu.
Mshindi huyo amepatikana miongoni
mwa mamilioni ya washiriki walioshiriki kucheza katika promosheni hiyo,
Katika mahojiano yaliyofanyika kwa njia ya simu Mshindi huyo ameishukuru
kampuni ya Vodacom kwa kumuwezesha kushinda kiasi hiko kwani hayakuwa
mategemeo yake katika maisha yake.
"Watu wengi hawakuwa wanaamini
kuwa Promosheni hizi ni za kweli, Sikuwa na pesa ya kucheza moja kwa
moja katika Promosheni hii ila nilipotumiwa pesa ya matumizi na mzee
niliamua kuweka na kushiriki katika Promosheni hii, Hakika nimefurahi
sana na ninawashukuru Vodacom, alisema Nickodemus.
Kwa upande wake mkuu wa kitengo
cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa
amewapongeza Wateja wa mtandao huo kwa kushiriki katika promosheni hiyo
na kumpongeza kwa upekee mshindi wa Promosheni hiyo na kujinasibu kuwa
anajivunia mafanikio ambayo Promosheni hiyo imeyapata kwa kufanikiwa
kubadili maisha ya mamia ya Watanzania.
"Sisi kama Vodacom tumefurahi kwa
kumpata mshindi wetu wa mwisho ambaye ameibuka kidedea kati ya Mamilioni
ya Watanzania lazima tukiri kuwa ni bahati kubwa na tunatoa pongezi za
kipekee kwa mshindi wetu, alisema Twissa na kuongeza kuwa "Zaidi ya yote
tunajivunia kwa upekee kabisa namna ambavyo promosheni hii imebadilisha
mamia ya maisha ya Watanzania, Tumepata washindi kutoka katika Nyanja
mbalimbali wakiwemo wakulima, wafanya biashara ndogondogo wanafunzi
pamoja na wastaafu wengi ambao nao wameendelea kuboresha maisha yao.
Tangu Promosheni ya MAHELA
kuzinduliwa tarehe 24 Mwezi wa kwanza na washindi 333 wamepatikana na
kushuhudia kiasi cha Shilingi milioni 480 zikitolewa hadi sasa.
No comments:
Post a Comment