SHIRIKA LA UNDER THE SAME SUN LATOA PONGEZI KWA UONGOZI WA MKOA WA RUKWA KWA KUFANIKIWA KUWAKAMATA WATUHUMIWA WALIOMKATA MKONO MLEMAVU WA NGOZI (ALBINO) NA KIZIBITI HICHO
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
Injinia
Stella Manyanya (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa
shirika
linalotetea haki za watu wenye ulemavu wa ngozi nchini (Albino) Vicky
Mketema
kulia na wajumbe wenzake wa shirika hilo watatu waliosimama nyuma. Kulia
waliosimama ni katibu wa Mkuu huyo wa Mkoa Frank Mateni na kushoto
aliyekaa ni
Afsa maendeleo ya jamii Mkoa wa Rukwa Deonisya Njuyui.
Mama Maria Chambanenge
mlemavu wa
ngozi anayenyonyesha mtoto wa miezi mitano alikatwa mkono na watuhumiwa
ambao
wameshatiwa nguvuni na jeshi la polisi Mkoa wa Rukwa na Mkono wake
uliokatwa
umeshapatikana. Upelelezi bado unaendelea kuwapata watuhumiwa zaidi
wanaohusika
na vitendo hivyo.
Mkurugenzi wa shirika la
under the
same sun Vicky Mketema ametoa pongezi za dhati kwa uongozi wa Mkoa wa
Rukwa kwa
kushughulikia tatizo hilo kikamilifu na kwa haraka na kufanikiwa kupata
kiungo
hicho na watuhumiwa waliohusika kwa muda wa siku mbili. Alisema endapo
mikoa
yote ingekuwa inashughulikia matatizo kama hayo kwa muda mfupi kama huo
basi
uhalifu na namna hii ungekuwa umeshatoweka nchini.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ametoa onyo kali kwa wale wote watakaohusika na vitendo vya uvunjifu wa amani Mkoani humo ambapo amewataka wananchi kutoa taarifa mapema kwa vyombo vya ulinzi pale wanapowashuku wahalifu wa vitendo hivyo. Amewato hofu wananchi kwani vyombo vya ulinzi na usalama vipo kwa ajili yo.
Muathirika huyo anaendelea kupata huduma za matibabu katika Hospitali Kuu ya Mkoa wa Rukwa na hali yake inaendelea vizuri.Picha Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa

No comments:
Post a Comment