RAIS WA ZANZIBAR DK ALI MOHD SHEIN AFUNGUA KATUO CHA KURUSHIA MATANGAZO YA DIJITALI ZANZIBAR




…………………………………………………….
Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar
SHIRIKA la Utangazaji Zanzibar
ZBC limetakiwa kuhakikisha kwamba linafanyakazi kwa ufanisi mkubwa
kulingana na mfumo uliopo hivi sasa.
Alisema kuwa wafanyakazi wa shirika hilo wameonakana wakifanya kazi kimazowea tu bila kufuata taratibu za kikazi.
Hayo yameelezwa leo na Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohammed Shein
katika Uzinduzi wa Miundombinu ya Dijitali na Jengo la Studio ya Kisasa Alisema kuwa kubadilika kwa watendaji kazi ni suala la lazima kutokana na mabadiliko makubwa yalioko duniani .
Dkt Shein alisema kuwa ZBC
wananchi wengi wanapiga kelele juu ya utendaji wa wafanyakazi wa ZBC
kutokana na vipindi vyao kutoridhisha na kukatika katika kwa matangazo
yao zaidi wakati wa taarifa ya habari.
Alisema kuwa Zanzibar inaheshima
yakekatika masuala ya Utangazaji kwani Redio nyingi za Nje
zinawatangazaji kutoka Zanzibar ambao ni mahiri katika masuala ya
Utangazaji.
No comments:
Post a Comment