Ilikuwa June 26.2007 tulipompoteza Mh. Amina Chifupa Mpakanjia. Ikiwa pia ni siku ya upigaji vita matumizi ya madawa ya kulevya.
Amina leo ametimiza Miaka Mitano sasa tangu alipotutoka na ataendelea
kukumbukwa kwa ucheshi wake, mbwembwe zake katika utangazaji wake
kupitia kipindi cha Chuchuchu, Kwa raha zetu, Bambataa na Leo tena
katika Redio ya Clouds FM.
Mpaka anakumbwa na mauti alikuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama
Cha Mapinduzi (CCM).Watanzania wataendelea kumuenzi na atakumbukwa kwa
vita yake dhidi ya wauzaji wa dawa ya kulevya.
Wakati leo tukimkumbuka Bi. Amina Chifupa, serikali nayo inaadhimisha Siku ya Kupambana na Dawa za kulenya Nchini.
Pumzika kwa Amani Amina Chifupa!
Chini ni picha za baadhi ya matukio mbalimbali ambayo Amina chifupa
aliweza kushikiriki wakati wa Uhai wake. Picha Hizi zilipigwa enzi hizo
na John Badi wa Daily Mitikasi Blog
|
No comments:
Post a Comment