BONGO MOVIE SHINYANGA YAMPONGEZA RAIS MAGUFULI SAKATA LA MADINI KWA KUMPA FILAMU HII FUPI "TANGANYIKA KARNE 18"
Kundi la Uigizaji wa Filamu ‘Bongo Movie Shinyanga’ limempongeza rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa hatua anazozichukua katika kulinda rasilimali za nchi hususani madini ya Tanzania.
Mwenyekiti wa Bongo Movie Shinyanga, Juma Songoro amesema rais Magufuli anapaswa kuungwa mkono na wananchi wote wa Tanzania na wazalendo wote.
"Wasanii wa filamu mkoa wa
Shinyanga tunampongeza sana rais Magufuli kwa hatua anazozichukua
kulinda nidhamu na rasilimali za nchi,tunamuombea kila la heri
atufikishe tunapopatarajia,tumeandaa filamu hii kama zawadi yetu kwake
na na watanzania wote",amesema Songoro.
Katika kufikisha pongezi hizo,Bongo Movie Shinyanga wameandaa Filamu fupi inaitwa 'Tanganyika Karne ya 18' inayoonesha jinsi nchi za nje zinavyoiba madini ya Tanzania.
TUMIKA DAKIKA ZAKO 3 TU KUTAZAMA FILAMU HII HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment