SERIKALI KUTUMIA BILIONI 435 KUTEKELEZA MIRADI YA KUPELEKA UMEME VIJIJINI.
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini Bw.Lutengano
Mwakahesya akitoa ufafanuzi kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali
ambapo zaidi ya Bilioni 435 zinatarajiwa kutumika kutekeleza miradi ya
kupeleka umeme katika maeneo mbalimbali hapa nchini lengo likiwa
kuwafikia watanzania wote. kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari
Maelezo bw. Frank Mvungi.
Meneja Wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Bw.
Elineema Mkumbo akitoa wito kwa watanzania kuunga mkono juhudi za
Serikali kufikisha nishati ya Umeme kwa watanzania wote kwa kushirikiana
na wadau mbalimbali. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati
Vijijini Bw.Lutengano Mwakahesya.
Frank Mvungi-Maelezo
SERIKALI
kutumia Bilioni 435 kutekeleza Miradi ya kupeleka Umeme Vijijini ikiwa
ni utekelezaji wa Malengo yakuhakikisha kila mtanzania anafikiwa na
nishati ya hiyo ili kukuza uchumi na kupanua wigo wa uzalishaji.
Kauli
hiyo imetolewa leo Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa
Nishati ya Umeme Vijijini (REA)Dkt. Lutengano Mwakhesya wakati wa
mkutano na waandishi wa Habari uliolenga kueleza hatua iliyofikiwa
katika kutekeleza miradi mbalimbali ya kupeleka umeme vijijini.
“Miradi
inayotekelezwa hadi sasa kwa awamu ya pili imekamilika kwa asilimia 90
na tunatumaini kuwa kasi ya utekelezaji wa miradi yote kwa awamu ya pili
na yatatu itakapoanza itaongezeka zaidi “ alisisitiza Mwakhesya.
Akifafanua
kuhusu idadi ya vijiji vilivyokwishanufaika Mwakhesya amesema kuwa
vijiji 5200 vimepatiwa umeme sawa na asilimia 36 ya vijiji vyote
vilivyopo hapa nchini ambavyo ni takribani 15,000.
Kwa
upande wa kiwango cha fedha zilizotolewa wakati wakala huo unaanzishwa
ni Bilioni 10 ambapo zimekuwa zikiongezaka mwaka hadi mwaka ili
kufikisha huduma hiyo kwa watanzania walio wengi zaidi.
Akizungumzia
Wilaya zilizonufaika na awamu ya kwanza Mwakhesya alizataja kuwa ni
Uyui,Kilolo Kilindi na Bahi ambapo kwa Sasa lengo ni kufikisha huduma
hiyo kwa wananchi wote.
Kwa
upande wake Meneja wa Wakala wa Nishati Vijijini Bw. Elineema Mkumbo
ametoa wito kwa watanzania kutumia fursa ya kuunganishiwa umeme kwa
gharama ya 27,000 tu lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa watanzania wengi
wanafikiwa na nishati hiyo.
No comments:
Post a Comment