NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO ASHUHUDIA KUORODHESHWA KWA HISA STAHILI ZA MAENDELEO BANK PLC, KATIKA SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM (DSE)
Naibu
Waziri wa Fedha na Uchumi, Dkt. Ashatu Kijaji, Mwenyekiti wa Maendeleo
Benki, Amulike Ngeliama (kushoto) na Mkurugenzi wa Tafiti, Sera na
Mipango wa(CMSA) Nicodemus Mukama wakifuatilia jambo katika hafla hiyo.
Naibu
Waziri wa Fedha na Uchumi, Dkt. Ashatu Kijaji akipiga kengele kuashiria
uorodheshwaji rasmi wa Maendeleo Benki katika soko la hisa DSE jana.
Kushoto ni Mwenyekiti wa Maendeleo Benki, Amulike Ngeliama na Mkurugenzi
wa Capital Markets na Securities Authoriy (CMSA) Nicodemus Mukama
Emmanuel Nyalali, Mkuu wa Kitengo cha Uendeshaji DSE akizungumza katika hafla hiyo.
Naibu
Waziri wa Fedha na Uchumi, Dkt. Ashatu Kijaji akiongea wakati wa hafla
ya kuorodheshwa kwa Maendeleo Benki katika soko la hisa DSE
Mkurugenzi
mtendaji wa Maendeleo Benki, Ibrahim Mwangalaba akitoa hotuba yake
kabla ya kumkaribisah Mwenyekiti wa Benki hiyo kuzungumza na washiriki
wa hafla hiyo.
Bank
PLC ni benki iliyoanzishwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania,
Dayosisi ya Mashariki na Pwani na inamilikiwa na Wananchi mbalimbali kwa
njia ya HISA bila kujali, kabila, itikadi, dini wala rangi, kwani benki
hii imesajiliwa na soko la hisa la Dar es Salaam (DSE), kupitia dirisha
dogo yaani Enterprise Growth Market (EGM) na inaendeshwa kwa kufuata
taratibu zote za BOT na Soko la Hisa la Dar es S alaam. Maendeleo Bank
ilianza kutoa huduma za kibenki tarehe 9/9/2013 baada ya kupewa leseni
na Benki Kuu ya Tanzania na tarehe 05/11/2013 ilisajiliwa rasmi katika
soko la hisa la Dar es Salaam baada ya kukidhi vigezo vyote vilivyowekwa
na mamlaka husika. Benki hii ilianza na mtaji wa shilingi bilioni 4.5
kutoka kwa wanahisa zaidi ya 3,000 wa rika na itikadi mbalimbali
walionunua wakati wa mauzo ya awali (IPO) yaliyofanyika mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment