NIA YA UDIWANI KATA YA SEGEREA NUSURA IMTOE ROHO MTOTO WA MASSABURI
Katibu wa Uchumi na Fedha Kata ya Segerea, Steve Massaburi akiwa Hospitali ya Aga-khan leo akiendelea na matibabu.
Katibu
wa Uchumi na Fedha Kata ya Segerea, Steve Massaburi akiwa Hospitali ya
Aga-khan leo akiendelea kuuguza majeraha baada ya kujeruhiwa kwa
mapanga nyumbani kwake Segerea jijini Dar es Salaam jana na watu
wasiojulikana. Kushoto anayemuhudumia ni jamaa yake Martin Pemba.
Na Dotto Mwaibale
WATU
wasiojulikana wamejeruhi kwa mapanga Katibu wa Uchumi na Fedha Kata ya
Segerea Steve Massaburi usiku wa kuamkia juzi nje ya nyumba yake
alipokua akirejea kutoka matembezini.
Kwa
mujibu wa Steve aliyelazwa katika Hospitali ya Aga khan, watu hao
wapatao wanne wakiwa na Pikipiki, walimvamia majira ya saa tatu usiku
nje ya geti la nyumba anayoishi na kuanza kumshambulia huku yeye
akijaribu kupambana nao.
Steve
ambaye ni mtoto wa Meya wa Jiji la Dar es salaam Dk. Didas Massaburi,
alisema wakati watu hao wakimshambulia walikuwa wakisema wazi wazi kuwa
lengo lao ni kumuona hagombei nafasi ya udiwani katika Kata hiyo ya
Segerea baada ya yeye kuonyesha nia ya kutaka kugombea nafasi hiyo.
“Walikuwa
wakiniambia kuwa wewe si unautaka udiwani sasa utaugombea ukiwa
kitandani au kaburini, hapa hakuna na umaharufu wa mtu kwa kuwa kila mtu
anaitaka nafasi hiyo” alisema Massaburi.
Alisema
wakati akiendelea kupambana na watu hao alikuwa akipiga kelele jambo
lililowafanya watu hao kumuacha na kasha kukimbia huku yeye akiwa
amelala chini damu zikimtoka sehemu za shavuni kutokana na panga
alilopigwa.
Pamoja
na sehemu ya shavuni, watu hao pia wamemjeruhi sehemu mbalimbali za
mkono wake wa kushoto alipokuwa akijaribu kuzuia panga kumdhuru sehemu
za usoni.
“Kelele
nilizopiga ndizo zilizonisaidia kwa kuwa ziliwafanya watu watoke katika
majumba yao kuja kunisaidia wakati huo huo watu hao wakikimbia kwa
kutumia pikipiki zao mbili walizokuwa wamekuja nao” aliongeza.
Alisema
kwa sasa hali yake inaendelea vizuri tangu alipofikishwa hospitalini
hapo jana huku akishonwa nyuzi zaidi ya ishirini katika taya lilipigwa
na panga na watu hao. (Imeandaliwa na mtandao wa www.
No comments:
Post a Comment