Historia ya John Magufuli wa CCM
Mgombea wa urais wa chama cha CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa
2015 Daktari John Pombe Joseph Magufuli ni mbunge wa jimbo la Chato
lililoko mkoa wa Geita na ni waziri wa ujenzi wa Tanzania.
Alizaliwa tarehe 29 Oktoba 1959 wilayani Chato Mkoani Kagera.
Kielimu, daktari Magufuli ana Stashahada ya elimu ya sayansi akibobea kwenye masomo ya Kemia, Hisabati.
Mgombea huyo wa urais ana shahada ya umahiri wa Sayansi na shahada ya uzamivu ya kemia.
Aidha
daktari Magufuli amewahi kufundisha katika shule ya sekondari Sengerema
miaka ya themanini kisha akajiunga na mafunzo ya JKT .
Alizaliwa Oktoba 1959
Alipohitimu, daktari Magufuli na aliaanza kufanya kazi katika
kiwanda cha ‘Nyanza Cooperative Union akiwa Mkemia kabla ya kuondoka
hapo na kuwania ubunge.
Magufuli alianza mbio za ubunge mwaka 1995
katika jimbo la Chato na kushinda kisha akateuliwa na Rais Benjamin
Mkapa kuwa naibu waziri wa Miundombinu.
Katika uchaguzi wa Mwaka wa 2000 pia aligombea ubunge na kushinda na Rais Mkapa akamteua kuwa Waziri wa miundombinu.
Alianza siasa mwaka 1995
Katika uchaguzi wa mwaka 2005 daktari Magufuli aligombea ubunge kwa mara ya tatu na kupita bila kupingwa.
Rais Kikwete alimteua kuongoza wizara ya Ardhi, nyumba na maendeleo ya
makazi na baadaye akamhamishia hadi wizara ya Mifugo na uvuvi.
Mwaka 2010 alichaguliwa kuwa mbunge kwa mara ya nne na Rais Kikwete alimrudisha katika Wizara ya Miundombinu na ujenzi.
Daktari
Magufuli anachukuliwa kuwa ni mwanasiasa mwenye msimamo thabiti,
mchapa kazi na asiye yumbishwa au hata kufuata upepo wa kisaisa.
Anatambulika kuwa Mchapa kazi
Watanzaniania wanamkumbuka kwa usimamizi na ujenzi wa barabara na majengo thabiti.
Anakumbukwa kwa kuchukua hatua za kutoa amri za kubomolewa kwa majengo ya kifahari ambayo alihisi yalikiuka sheria za ujenzi.
Na alipokuwa waziri wa Maendeleo ya Mifugo, Bwana John Magufuli
alikwenda hadi bandari ya Dar-es-Salaam na kuizuia meli ya wachina
iliyokuwa inashukiwa kufanya uvuvi haramu katika sehemu ya bahari ya
Tanzania.
No comments:
Post a Comment