Harambee ya ujenzi wa Kanisa la KKKT mkoani Rukwa – yafana
WAZIRI wa Maliasili na Utalii,
Lazaro Nyalandu, akijadiliana jambo na Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili
la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa (katikati) na Askofu
Ambele Mwaipopo wa Dayosisi ya Ziwa Tanganyika, wakati wa harambee ya
ujenzi wa Kanisa la KKKT mkoani Rukwa. Katika harambee hiyo Nyalandu,
aliyekuwa mgeni rasmi alichangia sh. Milioni 100. Harambee hiyo
ilifanyika jana usiku katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu
Julius Nyerere, Dar es Salaam.
ASKOFU Ambele Mwaipopo wa Kanisa
la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Ziwa Tanganyika,
akimkabidhi zawadi mbalimbali zilizotolewa na waumini wa kanisa hilo,
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, wakati wa harambee ya
kuchangia kanisa.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili
la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa, akimkabidhi zawadi
maalumu aliyopewa na Papa Francis XIV, Waziri wa Maliasili na Utalii,
Lazaro Nyalandu, ikiwa ni ishara ya kuthamini mchango wa sh. Milioni 100
alioutoa kuchangia ujenzi wa kanisa mjini Sumbawanga.
No comments:
Post a Comment