WAOMBA KITUO MAALUMU CHA WATOTO WALEMAVU BUHANGIJA KUSAIDIWA ZAHANATI.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Bi. Anne Rose Nyamubi mara
baada ya kuwasili ofisini kwake kwa ajili ya mazungumzo kabla ya
kuelekea kwenye kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum wakiwemo
walemavu wa ngozi cha Buhangija Jumuishi kilichopo mkoani Shinyanga.
Na mwandishi wetu, Shinyanga
MKUU
wa wilaya ya Shinyanga AnneRose Nyamubi ameomba jamii ya watanzania
kusaidia kupatikana kwa zahanati katika kituo cha kulelea watoto
walemavu cha Buhangija ili kupunguza adha wanazopata watoto hao katika
huduma za afya.
Kauli
hiyo ameitoa katika mazungumzo na mwandishi wa habari hizi ambaye
alifika katika kituo hicho akiambatana na ujumbe wa Umoja wa Mataifa
uliokuwa ukiongozwa na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na
mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini,
Alvaro Rodriguez.
Nyamubi
amesema kwamba ingawa hospitali ya mkoa ina dirisha kwa ajili ya
matibabu ya watoto hao,wakati mwingine inakuwa shida daktari maalumu
anayehusika anapokuwa hayupo. Aidha alisema kwa namna watoto hao walivyo
wanahitaji huduma ya karibu ya kitiba ambayo inawezekana kama kituo
hicho kingekuwa na zahanati yake.
Mkuu
wa Wilaya ya Shinyanga, Bi. Anne Rose Nyamubi akiwa kwenye mazungumzo
na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
aliyeambatana na Mshauri wa masuala ya haki za binadamu kutoka ofisi
kwake, Bi. Chitralekha Massey ( wa pili kulia kwake) pamoja na Mtaalam
wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu
(wa pili kushoto). Wengine katika picha ni Afisa Elimu Sayansikimu,
Beatrice Mbonea (wa kwa kulia), Afisa Elimu Msingi wa manispaa ya
Shinyanga, Bi. Pudensiana Magnus (katikati kulia), Mkurugenzi wa
manispaa ya Shinyanga, Festo Kang'ombe pamoja na Msaidizi wa Mkuu wa
Mkoa wa Shinyanga, Bw. Shadrack Kengese.
Kituo
hicho kilichoanzishwa mwaka 2010 kwa ajili ya watoto walemavu
wasiosikia na wasiiona kwa sasa kinapokea watoto wenye alibnizim ambao
wanaokabiliwa na ujahiri dhidi ya maisha yao. Kwa mujibu wa mkuu huyo wa
wilaya kituo hicho ambacho serikali hutenga bajeti kwa ajili ya
wanafunzi 50 wasiosikia na kuona, sasa kina watoto wenye albinism 247
ambao hawako katika bajeti na wanaishi kutokana na misaada ya watu
mbalimbali.
Alisema
kwamba watoto wenye albinism wanahitaji huduma za tiba za karibu zaidi
kutokana na mazingira yanawazunguka na dirisha pekee katika hospitali ya
mkoa halitoshi kwani wakati mwingine wanalazimika kukaa kwenye foleni
kama wagonjwa wengine na hili halipendezi.
Aidha
alisema kituo hicho cha Buhangija kwa sasa ni kidogo kuzingatia na
uwingi wa wanaohitaji msaada na hivyo serikali inatafuta eneo jingine
kwa ajili ya kujenga kituo.
Mazungumzo
yakiendelea ndani ya ofisi za Mkuu wa mkoa wa Shinyanga zinazokaimiwa
na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Bi Anne Rose Nyamubi.
Kufurika
kwa watoto hao wenye ulemavu kunatokana na tishio la maisha yao hasa
ukanda wa Ziwa ambapo familia zao zimewakimbiza kituoni hapo kwa ajili
ya usalama wao. Aidha Mkuu huyo wa wilaya amesema kwamba kituo hicho
hakina bajeti na kutaka wasamaria wema kuendelea kuchangia ili watoto
hao waendeshe maisha ya kawaida.
Naye
Mratibu wa Mashirika ya Umoja Mataifa yaliyopo nchini, Alvaro Rodrigues
amesema kwamba Umoja wa Mataifa utaendelea kusaidia kituo hicho na
kuwataka wanaotunzwa hapo kutoacha kuishi kama watoto kwani ndio tunu
waliyonayo kwa sasa.
Aidha
alisema kwamba anauchukua wimbo waliouimba ambao unazungumzia machungu
ya maisha yao na kwenda kuwaeleza watu wengine ili nao washiriki katika
kubadilisha hali ya kuogofisha na kuleta usalama.
Mkurugenzi
Mtendaji wa shirika la UNDER THE SAME SUN, Vicky Ntetema alijumuika
kwenye mazungumzo hayo. Pichani akifafanua jambo kwa Mratibu Mkazi wa
mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (hayupo pichani)
kuhusiana na changamoto mbalimbali zinazowakabili watu wenye ulemavu wa
ngozi nchini.
Alisema
wao (UN) wamefika katika kituo hicho kuona watoto wanavyoishi na
watafanya nini kuwasaidia. Aliwataka Watanzania kuhakikisha wanakomesha
machungu ya albino hao na kuishi nao kama watu wengine wa kawaida. Aidha
Mratibu huyo alipata nafasi ya kuzungumza na Binti wa miaka 19 Masabu
masuka ambaye amejifungua mwaka jana kituoni hapo bila msaada wa wauguzi
baada ya kulazimika kuondoka kwao akiwa mjamzito kukwepa mauaji dhidi
ya albino yaliyofanyika Mei mwaka jana wilayani Bariadi. Binti huyo
alifika kituoni hapo na kaka zake watatu ambao wote ni maalbino kama
yeye.
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga, Bi Anne Rose Nyamubi katika picha ya pamoja na
ugeni kutoka ofisi za Umoja wa Mataifa Tanzania na Shirika la UNDER THE
SAME SUN.
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga, Bi Anne Rose Nyamubi akiwasalimia watoto wenye
ulemavu wa ngozi wanaolelewa kwenye kituo cha Buhangija Jumuishi
kilichopo mkoani Shinyanga kabla ya kumtambulisha Mratibu Mkazi wa
mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (hayupo pichani).
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia)
akizungumza na watoto wenye ulemavu wakiwemo wa ngozi (hawapo pichani)
wanaolelewa kwenye kituo cha Buhangija Jumuishi kilichopo mkoani
Shinyanga alipofanya ziara ya kutembelea kituo hicho. Katikati ni
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania
Hoyce Temu na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Bi. Anne Rose
Nyamubi.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akitoa
zawadi ya maziwa kwa watoto wenye ulemavu wa ngozi wanaolelewa kwenye
kituo cha Buhangija Jumuishi kilichopo mkoani Shinyanga.
No comments:
Post a Comment