RAIS KIKWETE AREJESHA KIWANDA CHA CHAI CHA MPONDE,LUSHOTO MKOANI TANGA.

Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akihutubia katika mkutano ulioandaliwa
rasmi kuwaambia wananchi wa Mponde, Halmashauri ya Wilaya ya Bumburi,
Lushoto mkoani Tanga, kuwa Rais Jakaya Kikwete amekubali kukirudisha
Kiwanda cha Chai cha Mponde kwa wananchi baada ya mgogoro dhidi
mwekezaji wa kiwanda hicho, Yusufu Mula uliodumu kwa takribani miaka 10
na kusababisha kiwanda hicho kufungwa maiaka miwili iliyopita na
kuwaacha wananchi kwenye lindi kubwa la umasikini.
Hayo
ni Mafanikio ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman. Kinana ambaye katika
mkutano wa hadhara uliofanyika Septemba mwaka jana katika Kijiji cha
Mponde, aliahidi kupata suluhu ya mgogoro wa kiwanda hicho
ulioshindikana kutatuliwa kwa muda mrefu kwa kuupeleka kujadiliwa katika
Kamati Kuu ya CCM na kupata ufumbuzi ndani ya mwezi mmoja, ahadi ambayo
aliitimiza.
Kiwanda
hicho kilifungwa baada ya wananchi kususia kuendelea kulima mashamba ya
chai kwa lengo la kuishinikiza Serikali kutatua haraka mgogoro dhidi ya
Mwekezaji wa kiwanda hicho, Yusufu Mulla, ambaye walidai kuwa alikuwa
anawanyanyasa wakulima wa zao hilo pamoja na wafanyakazi kuwalipa ujira
mdogo.
Kinana
amesema Serikali itanunua hisa za mwekezaji ili aondoke na kuwaachia
wananchi kiwanda hicho.Pia Serikali itatuma jopo la wataalamu watakao
tathmini hasara iliyopo, na kutafuta mtaji wa kukifufua kiwanda ili
kianze kufanya kazi
Mbunge
wa Jimbo la Bumbuli,Mh. January Makamba akiishukuru Serikali kwa uamuzi
wake wa kukirudisha kiwanda hicho kwa wananchi ambapo pia alimshukuru
Rais Jakaya Kiwete na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman kwa kufanya
jitihada za kuhakikisha wananchi wanapata haki yao hiyo walioisotea kwa
takribani miaka 10.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa jimbo la
Bumbuli Mh. Januari Makamba wakati alipowasili jimboni humo katika
wilaya ya Lushoto, akiwa katika ziara ya siku mbili ambapo amefanya
mkutano wa hadhara katika kata ya Mponde na kuwataarifu wananchi na
wakulima wa Chai kuhusu maagizo ya Rais Jakaya Kikwete juu ya
kukirejesha kiwanda cha Chai cha Mponde kwa wananchi .
Baadhi ya Wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano huo wa hadhara wakisikiliza kwa makini.
Wananchi wa Bumbuli wakifuatilia mkutano wa hahara.
Mkutano ukiendelea katika uwanja wa Mponde,katika Halmashauri ya Bumbuli mkoani Tanga jioni ya leo.
Mkuu
wa Wilaya ya Lushoto,Mh.Majid Hemed akizungumza na Wananchi katika
mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo katika kijiji cha
Mponde,mkoani Tanga.
Baadhi ya Wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano huo wa hadhara wakisikiliza kwa makini
Mmoja
wa Wananchi akishangilia kwa namna yake mara baada ya Katibu Mkuu wa
CCM,Ndugu Kinana kutamka kuwa kiwanda cha Chai cha Mponde Rais Kikwete
ameamuru kilejeshwe mikononi mwa Wananchi na Wakulima wa Chai.
Wananchi wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo.
Mkuu
wa Mkoa wa Tanga,Magalulla Said Magalulla akiwasalimia na kujitambulisha
kwa wakazi wa Bumbuli na Vitongoji vyake,kwenye mkutano wa hadhara
uliofanyika jioni ya leo katika uwanja wa Mponde,Mkoani Tanga.
Mbunge
wa Jimbo la Lushoto na Mwenyekiti wa CCM Mkoa Tanga,Henry Shekifu
akifafanua jambo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo katika uwanja
wa Mponde,Mkoani Tanga.
No comments:
Post a Comment