MBUNGE WA MBEYA MJINI WA CHADEMA,MH JOSEPH MBILINYI A.K.A MR II APATA AJALI

Mbunge
wa Jimbo la Mbeya Mjini,Mh. Joseph Mbilinyi akifanya mawasiliano kwa
ndugu na jamaa mara baada ya kupata ajali mbaya na kunusurika kifo,ajali
hiyo imetokea eneo la Mlima Kitonga Mkoani Iringa mchana wa leo.kwa
mujibu wa chanzo chetu cha habari kimeeleza kuwa Mh. Mbilinyi alikuwa
safarini akitokea Mkoani Mbeya kuelekea jijini Dar akiwa na jamaa zake
Wanne katika gari hilo lenye namba za usajili T 148 BQE. katika ajali
hiyo hakuna aliyepoteza maisha.

Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini,Mh. Joseph Mbilinyi (watatu kushoto) akizungumza namna hali ilivyokuwa mpaka kupata ajali hiyo.

Gari hiyo inavyoonekana.

No comments:
Post a Comment