Ridhiwani
akizungumza jambo na Khamis Ibrahim baada ya mkutano kumalizika katika
Kijiji cha Kwaluhongo, wakati wa ziara yake ya kikazi katika Kata ya
Mbwewe, Chalinzi, wilayani Bagamoyo jana.
Mbunge
wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akihutubia wananchi katika
Kijiji cha Changarikwa wakati wa ziara ya kikazi pamoja na kuwashukuru
wananchi kwa kuchagua viongozi wa Seikali ya Kijiji wa CCM katika
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.CCM imepata ushindi wa Vijiji vyote katika
74 katika jimbo hilo.
Ridhiwani
akisisitiza jambo alipokuwa akihutubia katika kijiji hicho ambapo
aliwataka kuacha tabia ya kukata miti ovyo kwa ajili ya mkaa ama sivyo
vijiji vitageuka jangwa.
Mkazi
wa Kijiji cha Kwaluhongo, Dustan Sangi akiuliza swali kwa Mbunge wake
Ridhiwani Kikwete wakati wa mkutano uliofanyika kijijini hapo
Ridhiwani
akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kwaluhonbo
ambapo alijibu maswali mbalimbali ya wananchi kuhusiana na kero
mbaalimbali walizonazo pamoja na suluhisho
Mama mkazi wa Kijiji cha Changarikwa akiuliza swali kwa mbunge kuhusu tatizo la kijiji hicho kutokuwa na Zahanati
Katibu
wa CCM Wilaya ya Bagamoyo,Kombo Kamote akiwafunda viongozi wapya wa
Serikali ya Kijiji cha Changarikwa ambapo aliwataka kujali sana
maendeleo ya wananchi badala ya maslahi yao binafsi.
Wazee wakisikiliza kwa makini wakati Ridhiwani akihutubia katika Kijiji cha Changarikwa, Kata ya Mbwewe.
Ridhiwani
akiifariji familia ya marehemu Jangili Shaban alipokwenda kuhani msiba
baada ya kumalizika kwa mkutano katika Kijiji cha Changarikwa
Mzee Athuman Mnemwa akielezea mbele ya Mbunge wake Ridhiwani Kikwete jinsi Kijiji cha Kwang'andu kinavyoteseka na kero ya maji.
Mwanahawa
Habib akielezea mbele ya Ridhiwani jinsi wakazi wa kijiji hicho
wanavyonyapaliwa na Daktari na wauguzi wa Zahanati ya kijiji hicho
Mzee Athuman Kisuli akisisitiza umuhimu wa kupelekewa maji katika Kijiji cha Kwang'andu
Mbunge
wa Viti Maalumu Mkoa wa Pwani, Subira Mgalu akiwasalimia wananchi
wakati wa mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kwang'andu ambapo
aliahidi kusaidiana na Ridhiwani kutatua tatizo la maji linalowakabili
wananachi wa kijiji hicho
No comments:
Post a Comment