YALIYOJIRI KASHFA YA UCHOTWAJI BILIONI 360 IPTL YAMBABUA PINDA

Waziri Mizengo Pinda jana alijikuta katika wakati mgumu baada ya
kubanwa na wabunge ambao waliweka pembeni tofauti zao za vyama vya siasa
na kuungana kupinga vikali njama zinazodaiwa kufanywa na mahakama ya
Tanzania za kuingilia uhuru wa Bunge kulizuia kujadili ripoti ya
uchunguzi wa kashfa ya IPTL ya uchotwaji wa shilingi bilioni 360 katika
akaunti ya Tegeta Escrow iliyopo benki kuu ya Tanzania (BOT)
Hoja
za Wabunge hao zilionekana kulitikisa Bunge jana kiasi cha wabunge
kutotaka kusikiliza kauli ya serikali kupitia Waziri mkuu, Mizengo Pinda
kwani alipotoa ufafanuzi walisikika wakitoa matamushi ya
kutokukubaliana naye
No comments:
Post a Comment