KIJANA SANDE MWENYE KILO 250, AMEFARIKI DUNIA!

Kijana Sande Mrema aliyekuwa na tatizo la kuwa na kilo nyingi
zilizokuwa zikifikia 250 na umri wa miaka 25 aliyekuwa eneo la karakata
katika moja ya Hoteli alipokuwa akiishi wakati akisubiri kupatikana kwa
Ndege amefariki dunia usiku wa saa nne kuamkia leo jijini Dar es salaam.
Sande amefariki dunia wakati bado taratibu za kuona ni namna gani
atakavyoweza kupatiwa ndege kwaajili ya kwenda kupatiwa matibabu nchini
india zilikuwa zikifanyika miongoni mwa wanandugu.
Sande Mrema alishindwa kusafiri kwenda nchini india katika matibabu
yake baada ya kushushwa mara kadhaa kwenye ndege za kimataifa
anazotakiwa kusafiria licha ya ndugu zake kulipa Gharama zote za usafiri
wake.
R.I.P Sande
R.I.P Sande
No comments:
Post a Comment