Header Ads

MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA PILI WA KIMATAIFA KUHUSU LISHE NA VIRUTUBISHO JIJINI ROME, ITALIA NOVEMBA 21, 2014


  Papa Francis, akihutubia wakati wa mkutano huo....
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia Mkutano wa pili wa Kimataifa kuhusu Lishe na Virutubisho (ICN2) uliofanyika katika ukumbi wa Makao Makuu ya Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO) jijini Rome, Italia juzi Novemba 19, 2014.
  Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifuatilia hotuba mbalimbali za viongozi walioshiriki katika Mkutano huo wa ICN2. Kulia ni Mfalme Letsie III wa Lesotho.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Mpango Maalum wa Chakula Duniani (WFP) Ethria Cousin (kulia) na Balozi Wilfred Ngirwa wakati wa mkutano huo wa ICN2, uliofanyika juzi Novemba 19, 2014, Jijini Rome Italy.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijadiliana jambo na baadhi ya wajumbe kutoka Tanzania wakati wa mkutano huo wa ICN2 (kushoto) ni Balozi wa Tanzania nchini Italia, James Nsekela na Msaidizi wa Rais katika Masuala ya Lishe Dkt. Wilbald Lorri.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijadiliana jambo na baadhi ya wajumbe kutoka Tanzania wakati wa mkutano huo wa ICN2 (kushoto) ni Balozi wa Tanzania nchini Italia, James Nsekela na Balozi Wilfred Ngirwa (kulia).
 Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa FAO Jose Graziano da Silva, wakati alipomtembea ofisini kwake na kufanya naye mazungmzo, juzi Novemba 19, 2014. Kushoto ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashid. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
---
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA MAAKAMU WA RAIS
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal Novemba 19, 2014 ameiwakilisha Tanzania katika Mkutano wa Pili wa Kimataifa kuhusu Lishe na Virutubisho uliofanyika katika Makao Makuu ya Shirika la Kilimo na Chakula la 
Umoja wa Mataifa (FAO) jijini Rome Italia. 

Mkutano huu umefanyika ikiwa ni miaka 22 baada ya mkutano wa kwanza maarufu kwa jina la ICN1 kufanyika katika jiji la Rome na kuazimia kuwa, upo umuhimu wa kuhakikisha binadamu wanapata Lishe bora yenye virutubisho ili kusadia kujenga afya ya binadamu duniani. Mkutano huu wa pili pia umeandaliwa kwa pamoja na Shirika la Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO).

No comments:

Powered by Blogger.