KAMPUNI YA PAN AFRICAN ENERGY YATOA MSAADA WA MIFUKO 1500 YA SARUJI KWA WILAYA YA KILWA

Meneja
wa Uwajibikaji na Huduma za Jamii wa Kampuni ya uchimbaji wa gesi ya
Pan African Energy, Andrew Kashangaki (kwanza kushoto) akimkabidhi Kaimu
Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilwa Peter Malekela (kulia) msaada wa saruji
1,500 yenye thamani ya shilingi milioni 18 kwa halmashauri ya wilaya ya
Kilwa, Lindi ili kuwezesha ujenzi wa maabala 59 katika shule zake za
sekondari zipatazo 24. Pembeni wanaoshuhudia ni viongozi wa halmashauri
hiyo na wafanyakazi wa Kampuni ya uchimbaji wa gesi ya Pan African
Energy. Makabidhiano hayo yalifanyika mwanzoni mwa wiki Novemba 17, 2014
katika kiwanda cha Saruji cha Kilwa, Lindi. 


Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya Peter Amosi Malekela akizungumza machache.

Waandishi
wa habari wakifanya mahojiano na mwalimu wa masomo ya sayansi wa shule
ya sekondari Mtanda ambapo uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa na
viongozi toka kampuni ya Pan African Energy (T) Ltd.

No comments:
Post a Comment