Header Ads

HEBU ONA JINSI KATIBU MKUU WA CCM ABDULRAHMAN KINANA ALIVYOHITIMISHA ZIARA KWA KISHINDO LINDI


 Komredi Kinana akipandisha bendera wakati wa uzinduzi wa shina la Wakereketwa la CCM la Wanywaji wa  Kahawa mjini Lindi Jana
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Lindi jana, kuhitimisha ziara ya siku 8 katika Mkoa wa Lindi ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Lindi, ambapo amesema wapinzani wajiandae kupigwa mweleka katika uchaguzi wa Serikali za Mtaa Desemba 2014, akidai hawana mpango wa kuwaletea maendeleo wananchi.Pia amesema Mbunge wa Jimbo la Lindi Mjini Baruani wa CUF, ajiandae kung'oka akidai kodi yake imekwisha.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akishishiriki kuchimba  miundombinu ya maji katika Kijiji cha Mingoyo Mnazi Mmoja Lindi Mjini jana
 Kinana akiungana na wananchi kupapalia  katika shamba la kuzalisha mbegu bora za mihogo katika Kijiji cha Chikonji, wakati wa zaiara yake Wilaya ya Lindi Mjini.
 Kinana akisaidia kubeba zege za kujengea nyumba ya mwalimu katika Shule ya Msingi Nanyanje, Lindi Mjini.
 Kinana akishiriki kuvua samaki katika moja ya mabwawa 12  ya mjasiriamali Mjini Lindi
 Komredi Kinana akiwapungia mkono wananchi alipowasili kwenye mkutano wa hadhara mjini Lindi jana

No comments:

Powered by Blogger.