Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amesema kuwa hali ya afya yake inaendelea kuimarika. na kuwataka waumini kuendelea kumwombea.
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo
----
Na Goodluck Eliona, Mwananchi
Dar es Salaam.
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki,
Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amesema
kuwa hali ya afya yake inaendelea kuimarika. na kuwataka waumini
kuendelea kumwombea.
Akizungumza kwenye Misa Takatifu ya Mavuno na
shukurani kwa jimbo hilo, iliyofanyika jana Msimbazi Center jijini Dar
es Salaam, Pengo alisema ameamua kuitumia siku hiyo kumshukuru Mungu kwa
kuwa ndiye alimfanya kuwa hai hadi sasa.
“Namshukuru Mwenyezi Mungu, lakini pia
nawashukuruni nyote kwa sala zenu na dua zenu zilizoniwezesha hata
kusimama hapa mbele yenu saa hizi kama mnavyoniona,” alisema huku
akishangiliwa na mamia ya waumini wa kanisa hilo.
No comments:
Post a Comment