BREEEAKING NEWS,MKUDE ASAINI MIAKA MIWILI SIMBA SC
KIUNGO wa Simba SC, Jonas Gerald Mkude amesaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kuichezea Simba SC na kusema bado nipo sana…
KIUNGO wa Simba SC, Jonas Gerald Mkude amesaini mkataba wa miaka
miwili kuendelea kuichezea Simba SC na kusema bado nipo sana Msimbazi.
Akizungumza baada ya kusaini mkataba huo mbele ya waandishi wa habari
katika ukumbi wa Silver Pippe, Kawe, Dar es Salaam Mkude amesema kwamba
amesaini klabu hiyo baada ya kufikia kiwango cha fedha alichotaka.
Mkude mwenyewe hakusema ni kiasi gani amepewa, lakini habari ambazo
mtandao huu mezipata zinasema kiungo huyo amepewa Sh. Milioni 60, ingawa
mwenyewe alianzia Milioni 80.
No comments:
Post a Comment