Picha na Taarifa:Zaidi ya Taasisi 30 za Serikali hapa nchini zinatarajia kushiriki katika maonesho ya wiki moja ya utumishi wa Umma yanayotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 16 hadi 23 Juni katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
Naibu
Katibu Mkuu toka Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma HAB
Mkwizu (kulia) akisistiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)
mapema hii leo jijini Dar es Salaam juu ya maadhimisho ya siku ya
utumishi wa umma yanayotarajia kuanza tarehe16 Juni, kushoto ni
Mkurugenzi Idara ya Habari assah Mwambene.
Naibu
Katibu Mkuu toka Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma HAB
Mkwizu (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo
pichani) mapema hii leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumzia
maadhimisho ya Siku ya Utumishi wa Umma yanayotarajiwa kuanza Juni 16,
katikati ni Mkurugenzi Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu Bi. Roxana
Kijazi toka Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma na mwisho
kulia ni Mkrugenzi Msaidizi Idara ya Uchumi na Ushauri Kazi Bw. Hassan
Kitenge.
Jun
11
Tabasamu tu: Michael Richard
Wambura amemfunga bao tamu mwanasheria Dkt. Damas Ndumbaro baada ya
kamati ya Rufani ya TFF kumrudisha, sasa vita ni kati yake na Evanc
Aveva kwenye king`anyiro cha Urais katika uchaguzi wa juni 29 mwaka huu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Rufani za Uchaguzi ya
TFF, Julius Lugaziya (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar
es Salaam kuhusu uamuzi wa kamati hiyo kumrudisha mgombea wa Rais katika klabu
ya Simba, Michael Wambura. Kulia Mkurugenzi Msaidizi Sheria na Wanachama TFF,
Eliud Mvella.(Picha na Francis Dande)
Baadhi ya mashabiki wanaomuunga mkono mgombea wa
nafasi ya Rais wa klabu ya Simba, Michael Wambura wakishangilia nje ya ofisi za
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), baada ya kamati ya Rufaa ya TFF, kumrejesha
katika kinyang’anyiro hicho.Picha na Francis Dande
--
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
SAA chache baada ya Kamati ya
Rufani ya shirikisho la kandanda Tanzania, TFF, chini ya mwenyekiti
wake, Wakili Julius Mutabazi Lugaziya kumrudisha, Michael Richard
Wambura kwenye uchaguzi wa Simba sc, mgombea huyo amesema sasa haki
imetendeka na uchaguzi utakuwa wa amani.
Wambura amezungumza na mtandao
huu dakika chache zilizopita na kusema kuwa anaufananisha ushindi wake
kama mchezo wa mpira wa miguu.
No comments:
Post a Comment