Soma Kwa Makini Tamko Kutoka Ofisi Ya Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli-CCM Edward Lowassa ya Kulaaani Matendo ya Vikundi Vya Watu Kwenye Mitandao ya Kijamii Kumuhusisha Mheshimiwa Lowassa na Matukio ya Uongo na Mumzushia Vitu vya Ajabu Kabisa

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Edward Lowassa
---
Kumekuwa
na muendelezo wa matukio kadhaa kutoka kwa kikundi cha watu kumuhusisha
Mh Lowassa na matukio ya uongo na kumzushia vitu vya ajabu kabisa,
hususani katika mitandao ya kijamii.
Kumesambazwa
picha ya noti ya shilingi Mia tano yenye picha ya Mh Lowassa.Kitendo
hicho siyo Utani, bali ni dhihaka na dharau kwa alama za
utaifa na mamlaka ya nchi.
Mh Lowassa anaheshimu maoni ya watu na nguvu ya mitandao ya kijamii,
lakini anasisitiza umuhimu kwa wananchi kutumia nguvu hiyo ya mitandao
kwa kujadili maendeleo ya nchi yetu badala ya kuwa watu wa kuzusha mambo yasiyo na tija kwa nchi yetu.
Imetolewa na ofisi ya Mh lowassa(MB)
No comments:
Post a Comment