UNESCO YAITAKA SERIKALI KUZITAMBUA REDIO ZA JAMII NCHINI
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene
(kushoto) akiwasili katika Hoteli ya New Palm Tree iliyopo Bagamoyo
mkoani Pwani kufungua mkutano wa nne wa Mtandao wa vyombo vya habari vya
Kijamii nchini (COMNETA) akiwa ameongozana na wenyeji wake Afisa
Mipango Taifa wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari na mratibu wa miradi
ya UNESCO , Yusuph Al-Amin (wa pili kulia), Mwenyekiti wa COMNETA
ambaye pia ni Mkurugenzi wa Redio ya Jamii ya Wilayani Karagwe ya FADECO
Bw.Joseph Sekiku (wa pili kushoto) na Makamu Mwenyekiti wa COMNETA
ambaye pia ni Meneja wa Kituo cha Habari na Mawasiliano cha Telecentre
Sengerema FM mkoani Mwanza Bw. Felician Ncheye.
---
Na.Mwandishi wetu
SHIRIKA
la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni,(UNESCO), limeiomba
Serikali kutambua mchango wa redio za jamii katika maendeleo nchini na
hivyo kufanya nao kazi kwa karibu.
Ombi
hilo limetolewa jana na Afisa Mipango Taifa wa Kitengo cha Mawasiliano
na Habari na mratibu wa miradi ya UNESCO , Yusuph Al-Amin wakati wa
mkutano wa Mtandao wa vyombo vya habari vya Kijamii nchini (Community
Media Network of Tanzania – COMNETA)unaofanyika mjini Bagamoyo.
Akizungumza
kwenye mkutano huo, Al-Amin aliwapongeza COMNETA kwa kufanikiwa
kuanzisha umoja huo ambao awali kulikuwa na vituo viwili tu vilivyokuwa
vikitambuliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), huku kwa sasa
vikifikia vituo zaidi ya 27, kwa nchi nzima ikiwemo Tanzania Bara na
Visiwani.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene
akibadilishana mawazo na wenyeji wake kabla ya kufungua mkutano wa nne
wa COMNETA unaoendelea Bagamoyo mkoa wa Pwani.
Akifafanua
zaidi, Al-Amin alisema UNESCO imekuwa ukiisaidia COMNETA kufikia
malengo yake kwa kutambua kuwa radio hizo zinafanya kazi katika jamii
na zina uwezo mkubwa wa kuifikia jamii inayoizunguka.
“Zaidi
ya asilimia 70 ya Watanzania wako vijijini na hawa wanafikiwa kwa
karibu zaidi na radio jamii, kwa kupata taarifa za kina na za haraka”
alisema Al-Amin.
Alitoa
mfano wa Radio ya jamii iliyoko Micheweni, Pemba ambayo uwepo wake
umesaidia sana kuleta mabadiliko ya maendeleo wilayani hapo tofauti na
ilivyokuwa huko nyuma ambapo wilaya hiyo likuwa nyuma sana kimaendeleo.
‘Vipindi
mbalimbali vya kuhamasisha maendeleo vinavyorushwa na redio hii
vimesaidia sana kuhamasisha wananchi na sasa mwamko wa maendeleo umekuwa
mkubwa hapo Micheweni” alisema, Al-Amin.
Mwenyekiti
wa COMNETA ambaye pia ni Mkurugenzi wa Redio ya Jamii ya Wilayani
Karagwe ya FADECO Bw.Joseph Sekiku akizungumza na WanaCOMNETA kabla ya
kumkaribisha mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah
Mwambene.
Aliwashauri
wanachama wa COMNETA, wawe na umoja, mshikamano na kupendana ili
kuepuka migogoro inayoweza kuyumbisha ustawi wa chama. “Tunawaomba sana,
COMNETA, muwe mfano wa kuigwa kwa kuepuka migongano ya wenyewe kwa
wenyewe ikiwamo kugombea madaraka ili kuwa umoja wa mfano kwa katika
tasnia ya vyombo vya habari hapa nchini’.
Kwa
upande wake, mgeni rasmi katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Idara ya
Habari (MAELEZO) Assah Mwambene aliupongeza umoja huo na kuwataka
kuendelea kuwa daraja muhimu la kuipasha jamii mambo yote ya msingi bila
kuvunja misingi ya kitaifa ikiwemo kulinda maslahi ya taifa.
“Kwanza
kabisa, niwapongeze, COMNETA kwa kuanzisha umoja wenu huu, na kuwapo
kwangu hapa leo kunanifunza mengi, hivyo kwa yale yote mulioniomba
nami, nitayafikisha kwa wahusika na kuyafanyia kazi” alisema, Mwambene.
Aidha,
akijibu maswali mbali mbali ya wajumbe yaliyokuwa yakitolewa kwenye
mkutano huo, Mwambene aliwahakikishia kuwa Serikali inatambua mchango wa
vyombo vya habari na inatarajia kupeleka muswada wa sheria ya vyombo
vya habari kwenye Bunge lijalo.
“Muswada wa habari upo tayari, tunatarajia utapelekwa Bungeni katika
kikao kijacho mwezi Desemba ili kujadiliwa.Tunaamini Kamati husika ya
Bunge itawakaribisha wadau wa tasnia ya habari ili kutoa mawazo yao
katika muswada huo kabla haujafikishwa bungeni,” alisema.
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene akitoa risala wakati
akifungua mkutano wa siku nne wa COMNETA unaoendelea mjini Bagamoyo mkoa
wa Pwani.
Akidokeza
juu ya yaliyomo ndani ya muswada huo, Mwambene alisema umebainisha wazi
ulazima wa wamiliki wa vyombo vya habari kuwakatia bima za afya na
usalama kazini waajiriwa wao pamoja na suala la maslahi stahiki kwa
waandishi wa habari. Muswada huo pia umependekeza kiwango cha elimu kwa
mwandishi wa habari kiwe shahada ya kwanza.
Kwa
upande wake, Makamu Mwenyekiti wa COMNETA, Bw. Felician Nchewe aliomba
Serikali ivifikirie vyombo vya Jamii nchini, katika kufikia malengo
yake.
Afisa Mipango Taifa wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari na mratibu wa
miradi ya UNESCO, Bw.Yusuph Al-Amin akizungumza mbele ya mgeni rasmi
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) wakati wa ufunguzi wa mkutano wa
nne wa WanaCOMNETA uliofunguliwa rasmi jana wilayani Bagamoyo mkoa wa
Pwani.
“Kwa
sasa COMNETA, tumefikia malengo mbali mbali, hivyo tunaiomba sana
Serikali ivifikie vyombo hivi vya Jamii, kama ilivyo kwa wenzetu kupitia
TCRA, kuvisaidia vituo vya Tele Centre kufikia malengo yao” alisema
Nchewe.
Kwa
upande wake, Mkufunzi wa radio za Jamii kutoka UNESCO, Mama Rose Hajj
Mwalimu alisema mkutano huo wa COMNETA wa siku nne, ni wa kuweka mifumo
na mikakati bora ya uendashaji wa vituo hivyo na kuweka maazimio ya
kufanyia kazi. Ambapo uliwahusisha Mameneja na Wakurugenzi kutoka radio
za Jamii (Community Radio) zilizopo nchini.
Mkutano huo unaendelea katika hoteli ya New Palm Tree Village, Bagamoyo.
Meneja wa Redio Kahama FM Marco Mipawa akichangia maoni yake juu ya
sheria ya Magereza wakati wa mkutano wa nne wa COMNETA unaohusisha redio
za Jamii nchini uliofadhiliwa na Shirika la UNESCO kupitia mradi wa
DEP.
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama akitoa maoni yake katika mkutano huo
Baadhi
ya washiriki wakisikiliza mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa wakati
wa mkutano wa nne wa COMNETA unaoendelea Bagamoyo mkoani Pwani.
Erick Kalunga kutoka Ubalozi wa Uswiss ambao wanadhamini mradi wa SIDA
akizungumzia furaha yao kuona miradi wanayofadhili inapiga hatua na
kuleta maendeleo kwa jamii.
Mwenyekiti wa Tanzania Telecentre Network (TTN) Bw. Hirnoy Barmeda akizungumzia umuhimu wa Telecentre kwa jamii.
Mkurugenzi
wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Barmedas na Jamii Foundation Crystal
Kigoni akifafanua kuhusu taasisi yao isiyo ya Kiserikali
inayojishughulisha na mambo ya ustawi wa Jamiikupitia vyombo vya habari
na Teknohama kwa kuibua mambo yanayotokea mitaani kwa jamii
inayozunguka Redio za Jamii.
Washiriki wa mkutano wa nne wa COMNETA unaoendelea wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Mkutano wa nne wa WanaCOMNETA ukiendelea katika hoteli ya New Palm Tree wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani.
Mratibu
wa Mtandao wa Jinsia na Habari Tawi la Tanzania (GEMSAT) Bi. Gladness
Hemedi Munuo akiongelea usawa wa jinsia katika Uongozi na Utawala kwa
Redio za Jamii.
Mshauri wa UNESCO, Balozi mstaafu Mh. Celestine Liundi akisisitiza umuhimu wa kuhubiri amani kwa redio za Jamii nchini.
Meneja
wa mradi wa DEP kutoka UNESCO Courtney Ivins akibadilishana mawazo na
Mwenyekiti wa COMNETA ambaye pia ni Mkurugenzi wa Redio ya Jamii ya
Wilayani Karagwe ya FADECO Bw.Joseph Sekiku kwenye mkutano wa
WanaCOMNETA unaoendelea wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani.
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene katika picha ya pamoja
na WanaCOMNETA mara baada ya kufungua mkutano wa nne wa COMNETA wilayani
Bagamoyo.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene katika picha ya pamoja na Bodi ya COMNETA.
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene (kulia) akibadilishana
mawazo na Mshauri wa UNESCO, Balozi mstaafu Celestine Liundi (katikati)
pamoja Mkufunzi wa Mafunzo hayo ambaye pia ni Mjumbe ya wadhamini
COMNETA Bw. Gervas Mushiro (kushoto)
No comments:
Post a Comment