Mfanyabiashara wa magari, Gabriel Munisi jana alivyojiua baada ya kumuua mtu mmoja na kujeruhi wengine watatu jijini Dar es Salaam katika tukio linalohusishwa na wivu wa mapenzi.

Polisi wakikagua gari walilokuwa wakisafiria watu wanne kabla ya
kushambuliwa kwa risasi na mtu alitajwa kuwa jina la Gabriel Munisi
aliyedaiwa kuua watu wawili na yeye kujiua baada ya kujeruhi wengine
jana asubuhi jirani na Club ya Wazee, Ilala, jijini Dar es Salaam. Picha
ndogo polisi wakikagua silaha iliyotumika.Picha na Silvan Kiwale
-----
Mfanyabiashara wa magari, Gabriel Munisi (35), jana alijiua
baada ya kumuua mtu mmoja na kujeruhi wengine watatu jijini Dar es
Salaam katika tukio linalohusishwa na wivu wa mapenzi.
Munisi, ambaye alikuwa mkazi wa Mwanza, aliwapiga
risasi watu watatu akiwamo mchumba wake, Christina Alfred katika Mtaa wa
Bungoni Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam.
Baada ya kumpiga risasi mchumba wake huyo na
kudhania kwamba amemuua, inadaiwa kwamba Munisi aliendelea kuwamiminia
risasi watu wengine na kumuua mdogo wake Christina, Alpha (22).Kwa habari zaidi Bofya na Endelea.........
No comments:
Post a Comment