PSPF YATAMBULISHA MPANGO WA UCHANGIAJI WA HIARI (PSS) KWA WAANDISHI WA HABARI
Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji PSPF ambaye pia ni
Meneja wa kumbukumbu, Chacha Nyaikwabe
Kutoka kushoto ni Afisa Mawasiliano, Masoko na
Uenezi wa PSPF, Hawa Kikeke, Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji PSPF ambaye pia ni
Meneja wa kumbukumbu, Chacha Nyaikwabe na Frank Mvungi wa Maelezo wakati PSPF
ilipozungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa habari maelezo
Waandishi wa habari wakisikiliza ufafanuzi kuhusu
mfuko wa pensheni PSPF.
Kutoka kushoto ni Afisa Mawasiliano, Masoko na
Uenezi wa PSPF, Hawa Kikeke, Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji PSPF ambaye pia ni
Meneja wa kumbukumbu, Chacha Nyaikwabe
---
Waandishi wa habari nchini wameshauriwa kujiunga
na mpango wa uchangiaji wa hiari (PSPF Supplementary Scheme PSS) katika Mfuko
wa pesheni wa PSPF ili kujiwekea akiba yenye mafao bora na itakayowainua
kiuchumi.
Wito huo umetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa
Uendeshaji PSPF ambaye pia ni Meneja wa kumbukumbu, Chacha Nyaikwabe wakati
akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa habari maelezo Novemba 19
mwaka huu.
Nyaikwabe amesema mpango wa uchangiaji wa hiari
ni msaada mkubwa kwa watu wote walio na wasio katika sekta rasmi ambao kwa
kujiunga na mpango huo watanufaika na mafao ya elimu, ugonjwa, ujasiliamali,
fao la uzeeni, kujitoa na mkopo wa nyumba kwa wale watakaokidhi vigezo.
“PSPF sasa ni kwa watu wote walio kwenye sekta rasmi na wale ambao
hawako kwenye sekta rasmi maana lengo letu ni kuwafikia watu wengi ndani na nje
ya nchi kupitia mpango huu wa uchangiaji wa hiari PSS ambao kiwango chake cha
chini cha uchangiaji ni sh.10,000 kwa mwezi” anasema Nyaikwabe.
Akizungumzia mwamko wa watu kujiunga na mpango
huo wa hiari PSS, Nyaikwabe amesema kumekuwa na mafanikio makubwa kwani tangu
kuzinduliwa kwake mapema machi 7 mwaka huu tayari wanachama zaidi ya 2000
wamejiunga na mpango huo.
Kwa upande wake Afisa Mawasiliano, Masoko na
Uenezi wa PSPF, Hawa Kikeke watu wengi wanajiunga na mfuko huo kutokana na
ubora wa mafao yake na mikopo inayotolewa kwa wanachama waliojiunga na mfuko
huo kwa miaka mitano tofauti na wakati wa nyuma ambapo mikopo ya nyumba
ilitolewa kwa wanachama waliobakiza miaka mitano ya kustaafu.
No comments:
Post a Comment