CHAMA CHA WALIMU CWT CHATOA TAMKO LAKE KWA SERIKALI
Rais
wa Chama Cha walimu Tanzania Bw. Gratian Mukoba (Kushoto) akiongea na
waandishi wa habari leo katika makao makuu ya Chama hicho jijini Dar es
Salaam kuhusiana na Tamko lao kwa serikali kutaka iwarudishie madaraka
wakuu wote waliovuliwa nyadhifa zao kwakuwa ni viongozi wa (CWT) ndio
waliohamasisha mgomo.
Vilevile
chama hicho kimeitaka serikali kufuta nia yake ya kuwashitaki walimu
zaidi ya 180,000 walioshiriki mgomo kati ya walimu 233,440 walioko
nchini kwani kwa kufanya hivyo watoto wa maskini wanaotegemea walimu hao
kufundisha watakosa haki yao ya kufundishwa.Kulia na Kaimu katibu mkuu
wa chama hicho Bw, Ezekiel Olotu.
(PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)
)Baadhi
ya Waandishi wa habari waliohudhuria katika mkutano huo wakifuatilia
taarifa iliyokuwa ikitolewa na Rais wa Chama cha walimu CWT nchini.


No comments:
Post a Comment