TUME YA PAMOJA YA KUDUMU YA USHIRIKIANO BAINA YATANZANIA NA RWANDA YAFANYA KIKAO CHAKE GISENYI RWANDA
Gisenyi RWANDA
Kikao cha
Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda
kilichofanyika kuanzia tarehe 29 – 30 Aprili, 2016,kimekamilika Mjini
Gisenyi, Rwanda,ambapo wataalam wa sekta mbalimbali wameazimia
kuharakisha maeneo ya ushirikiano baina ya nchi hizi mbili.
Kikao
hicho cha 14 cha ushirikiano kimefanyika kufuatia maagizo ya Marais wa
Tanzania na Rwanda wakati wa ziara ya Mhe. Dkt. John PombeMagufuli
nchini Rwanda mwanzoni mwa mwezi Aprili mwaka huu.
Wakati wa
ziara hiyo,wakuu hao walikubaliana kuharakisha utekelezaji wa
makubaliano ya ushirikiano na kuibua maeneo mapya yanayolenga kuinua
shughuli za kiuchumi baina ya nchi hizo mbili.
Wakati wa
ufunguzi wa kikao hicho cha wataalamu kiongozi wa ujumbe wa Tanzania
Balozi Ramadhan M. Mwinyi, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Njeya
Tanzania aliwakumbusha wajumbe wa pande zote mbili kuendesha mazungumzo
na mjadala kwa kuzingatia maagizo ya viongozi hao na vilevile
kuchangamkia fursa za ushirikiano wa shughuli za kiuchumi za wananchi wa
pande zote mbili baada ya mindombinu ya kikanda kuimarika.
Kwau
pande wake, Balozi Jeanine Kambanda, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Njeya Rwanda na mwenyeji wa kikao hicho, alihimiza wajumbe kujiwekea
malengo yanayotekelezeka na tarehe za ukomo kwenye maeneo yote
watakayokubaliana ili kusukuma utekelezaji na kupata matokeo ya haraka.
Pamoja na
mambo mengine, pande zote mbili zimekubaliana kuimarisha ushirikiano
katika sekta muhimu kama vile miundombinu ya ushorobawakati (Central
Corridor), kuharakisha ujenzi wa reli ya kati katika kiwango cha
kimataifa (Standard Gauge), kukuza ushirikiano katika sekta ya anga
hususan baina ya mashirika ya ndege ya Rwandair na ATCL, kuimarisha
ushirikiano katika sekta za sayansi na teknolojia, afya, kilimo na
ufugaji, utalii, elimu, mawasiliano n.k.
Mkutano
huo pia umekubaliana kuanzisha Kamati yaPamoja ya Utekelezaji (Joint
Implementation Committee) kwa ajili ya kufuatilia kwa karibu maeneo yote
ya ushirikiano yaliyokubaliwa katika Kikao hicho cha 14. Kamati hiyo
itakayoongozwa na Makatibu Wakuu wa Wizara za Mambo ya Nje za nchi hizo
mbili, itakutana kila robo mwaka.
Aidha,
Serikaliya Rwanda imeonesha utayari wake wakuleta nchiniMaafisa na
Watumishi waSerikali kwalengo la kupata uzoefu na mafunzo katika vyuo
vya kitaalamu nchini kama vile Chuo cha Diplomasia (CFR), Chuo cha
Taifa cha Utalii na Wanyamapori (Mweka) na Chuo cha Usafirishaji (NIT).
Kwa
upande wa Tanzania, Serikali imedhamiria kuwakutanisha wataalamu wa
mitaala ya elimu kwa lengo la kubadilishana uzoefu na Rwanda kwenye
upande wa kuandaa mitaala ya elimu ya tehama kwenye shule za awali,
msingi na sekondari.
Mkutano
ujao wa kuminatano waTume ya Pamoja yaKudumu ya Ushirikiano kati ya
Tanzania na Rwanda utafanyika mwaka 2018, nchini Tanzania.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa,
30 Aprili, 2016
Gisenyi RWANDA
No comments:
Post a Comment