UTT-PID YASHIRIKI MAONYESHO YA SABASABA NDANI YA BANDA LA WIZARA YA FEDHA


Afisa
Masoko Bi. Kilave Atenaka (Kulia) wa Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya
Miundo Mbinu iliyochini ya Wizara ya Fedha (UTT –PID) akiwasikiliza
wateja waliotembelea katika banda kwenye maonyesho ya 39 ya Biashara ya
Kimataifa, Dar es Salaam yanayoendelea katika mabanda ya Saba Saba
katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ndani ya banda la
Wizara ya Fedha.

Afisa
Masoko Bi. Kilave Atenaka (Kushoto) wa Taasisi ya Miradi na Maendeleo
ya Miundo Mbinu iliyochini ya Wizara ya Fedha (UTT –PID) wakiwa na
nyuso za furaha na Bi. Beatrice Ngoda katika banda kwenye maonyesho ya
39 ya Biashara ya Kimataifa, Dar es Salaam yanayoendelea katika
mabanda ya Saba Saba katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere ndani ya banda la Wizara ya Fedha.

Afisa
Masoko Bi. Mary Minja (Kulia) wa Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya
Miundo Mbinu iliyochini ya Wizara ya Fedha (UTT –PID) akimsikiliza mteja
aliyetembelea katika banda kwenye maonyesho ya 39 ya Biashara ya
Kimataifa, Dar es Salaam yanayoendelea katika mabanda ya Saba Saba
katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ndani ya banda la
Wizara ya Fedha.


Taasisi
ya Miradi na Maendeleo ya Miundo Mbinu iliyochini ya Wizara ya Fedha
(UTT –PID) ipo kwenye maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa, Dar es
Salaam yananoendelea katika mabanda ya Saba Saba katika Viwanja vya
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Banda
la UTT PID lipo jirani na kuingia katika Banda la Wizara ya Fedha upande
wa kulia… karibuni sana wananchi mnaombwa kujitokeza kwa wingi mjipatie
huduma mbali mbali zinazotolewa na taasisi hiyo ikiwemo huduma za
uuzwaji wa viwanja katika maeneo mengi ya nchi ikiwemo vile vya mradi wa
katika Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundo Mbinu iliyochini ya
Wizara ya Fedha (UTT–PID) miji ya Chalinze na Bagamoyo mkoani Pwani.
Akielezea
Afisa Masoko Bi. Kilave Atenaka alisema kuwa kwa sasa wanaendesha
huduma ya uuzwaji wa Fomu kwa ajili ya Viwanja, pia wanatarajia kuanza
kuuza kwa umaa na taasisi mbali mbali miradi mipya ikiwemo wa Tundwi
Songai – Kigamboni jijini Dar es Salaam na ule wa Kingorwila, Morogoro.
Aidha
Bi. Kilave alitumia wito huo kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi
ndani ya banda hilo kujipatia elimu mbali mbali zitolewazo na taasisi
hiyo hapa nchini. Kwa sasa UTT PID ni miongoni mwa taasisi zinazofanya
vizuri katika utoaji huduma za ushauri katika maeneo ya upembuaji
yakinifu wa miradi mbali mbali, uratibu wa fedha na huduma zinazohusian
katika maandalizi ya mapendekezo ya miradi kwa benki au taasisi za
fedha, uteuzi wa watoa huduma kuhusiana na maandalizi y a zabuni na
usimamizi wa majengo na mali ambao ni utoaji wa huduma fanisi za usimizi
wa majengo yaliyochini ya uangalizi thabiti wa taasisi.
No comments:
Post a Comment