Header Ads

PUSH MOBILE, UN , WIZARA KUKABILI EBOLA

FullSizeRender
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (katikati) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Push Mobile, Freddie Manento (kushoto) wakitiliana saini makubaliano ya ushirikiano wa kukabiliana na ugonjwa wa ebola kwa kutoa elimu kwa jamii kupitia ujumbe mfupi maneno katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ofisi za Mratibu mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa jijini Dar. Anayeshuhudia tukio hilo ni Mwakilishi wa UNICEF Tanzania, Dkt. Jama Gulaid.(Picha na Umoja wa Mataifa).

KAMPUNI ya simu ya Push Mobile imetiliana saini na serikali ya Tanzania na Umoja wa Mataifa (UN) ya kuwafikia watu milioni 10 ikiwahabarisha kuhusu ugonjwa hatari wa ebola.

Kwa mujibu wa taarifa ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa mjini hapa kampuni hiyo ya simu imesema kupitia ushirikiano huo kampuni hiyo ya simu itaunga mkono juhudi za serikali ya Tanzania na Umoja wa Mataifa wa kutoa elimu dhidi ya ugonjwa huo ujumbe mfupi utakaoelezea ugonjwa wa ebola.

Kama sehemu ya makubaliano, Push Mobile , UN, serikali na wadau wake watatoa taarifa kuhusu ugonjwa huo wanapohitajika. Watanzania wanaweza kupata habari za ugonjwa huo kwa kuandika neno EBOLA kwenye namba 15774 na kupata taarifa za ugonjwa huo bure bila kutozwa gharama.
IMG_8005
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Push Mobile, Freddie Manento wakionyesha hati za makubaliano ya ushirikiano huo.

Wakitia saini Ofisa Mtendaji Mkuu wa Push Mobile, Freddie Manento amesema kwamba kama Ujumbe mfupi unaweza kuokoa maisha kampuni yake iko tayari kushiriki katika kampeni hiyo.

No comments:

Powered by Blogger.