Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe amesema atamuunga mkono Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani, Freeman Mbowe pale atakapowasilisha hoja yake bungeni kuhusu ufisadi wa zaidi ya Sh1 trilioni katika mradi wa bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam.

HAKI SAWA: Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba (kulia) na
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Zitto Kabwe
wakiwasili kwenye Uwanja wa Mashujaa mjini Mtwara jana, ambako
walihutubia mkutano wa hadhara. Picha na Ibrahimu Yamola
---
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za
Serikali (PAC), Zitto Kabwe amesema atamuunga mkono Kiongozi wa Kambi
Rasmi ya Upinzani, Freeman Mbowe pale atakapowasilisha hoja yake bungeni
kuhusu ufisadi wa zaidi ya Sh1 trilioni katika mradi wa bomba la gesi
kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam.
Zitto aliyasema hayo jana katika mkutano wa
hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa mkoani hapa uliandaliwa na
Chama cha Wananchi (CUF) kuwashukuru wakazi wa mkoa huo kwa kuwachagua
viongozi wa chama hicho katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
“Najua bado mnalia kuhusu bomba la kupeleka gesi
Dar es Salaam, machozi yenu yatafutika kwani tayari habari za ufisadi
mkubwa katika ujenzi wa bomba hili zimeanza kuchomoza.
“Kiongozi wa Upinzani Bungeni (Mbowe) ametamka
mara kadhaa kuwa atatoa hoja kuhusu ufisadi katika ujenzi wa bomba la
gesi. Pale atakapohitaji msaada wetu tutamsaidia, tunaamini gharama za
mradi huu zimezidishwa mara mbili na inawezekana kabisa kuwa zaidi ya
Dola ya Marekani 600 milioni (zaidi ya Sh1 trilioni) zimegawanywa kwa
watu kama rushwa kuanzia China mpaka hapa Tanzania. Machozi yenu wana
Mtwara yatafutwa kwa uwezo wa Mola,” alisema Zitto.
Alisema katika miaka ya hivi karibuni Mkoa wa
Mtwara umechukua sura mpya kitaifa baada ya kugunduliwa kwa gesi na wao
(wananchi) wameonyesha kwamba wakiamua wanaweza kupigania masilahi ya
Taifa.
“Mmesimama kidete kuhakikisha utajiri huu hauporwi
na haturudii makosa yaliyofanyika Kanda ya Ziwa pale tuliporuhusu
madini kuporwa na mabeberu wa kimagharibi,” alisema.
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba
akiwahutubia wakazi hao, aliwataka viongozi wa Serikali za Mitaa
waliochaguliwa kuongoza kwa misingi ya chama ya haki sawa kwa wote.Kwa Habari Zaidi Bofya na Endelea.....
No comments:
Post a Comment