Header Ads

RAHA YA MAFANIKIO YAKO USAIDIE NA WENGINE WAFANIKIWE!

Mpenzi msomaji wangu, unapojaaliwa kuwa na mafanikio jambo la kwanza unatakiwa kumshukuru sana Mungu pamoja na wale ambao kwa namna moja ama nyingine wamekufanya ufike hapo ulipo.Huwezi kufanikiwa kwa ujanja wako, mafanikio yako yote nyuma yake kuna mkono wa Mungu. Yeye ndiye anayeweza kuziona jitihada ulizonazo na akaona akutimizie ndoto zako.
Ukiacha yeye, wapo watu mmojammoja au kwa vikundi na taasisi ambao wamechangia wewe kuwa na mafanikio uliyo nayo. Hawa ni watu wa kuwaheshimu sana. Kamwe usiwasahau, endelea kuwa nao karibu kwani umuhimu wao kwako ni mkubwa sana.
Aidha, unapofanikiwa na wewe unatakiwa kuwa chachu ya mafanikio kwa wengine. Unatakiwa kuwashika mkono ndugu, marafiki na watu wengine wanaokuzunguka ili watoke kwenye hali duni walizonazo. Ukifanya hivyo utazidi kupaa kimafanikio…

No comments:

Powered by Blogger.