Header Ads

Tutengeneze Katiba inayolenga kutatua matatizo ya wananchi wetu kwa miaka 50 ijayo: Prof. Mwandosya.

 Mjumbe wa Bunge Maalum, Mhe. Prof. Mark Mwandosya akichangia mjadala wa ndani ya Bunge Maalum kujadili taarifa za kamati za bunge hilo zilizowasilishwa wiki iliyopita kwa ajili ya kuandika Katiba inayopendekezwa.(Picha na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma)
 
Na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma.
 
MJUMBE wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Prof. Mark Mwandosya ameeleza kuwa mpaka ifikapo mwaka 2055 Tanzania itakuwa imeachana na umaskini katika nchi ya uchumi wa kwanza endapo kutakuwa na dhamira ya dhati hususani kuwa kuandika Katiba yenye kuleta nafuu kwa watanzania kwani kila kitu kwa Waafrika kinawezekana pasipo kuwa na Wazungu.
 
Prof. Mwandosya alisema hayo jana wakati akichangia mjadala wa katiba ndani ya Bunge Maalum, ambapo alisisitiza umuhimu wa kuwa na katiba itakayozingatia vipaumbele ambavyo vinaweza kumkwamua mwananchi wa kawaida kuondokana na umasikini na kuliinua Taifa kiuchumi.
 
Mhe. Mwandosya amesema kuwa kuhusu changamoto na kero zinazohusu mambo ya Muungano, katiba imejaribu kuzizingatia karibia zote, huku akieleza kuwa hali ya Muungano ni imara na itaendelea kuwa imara.

No comments:

Powered by Blogger.