Mkutano wa 29 wa Baraza la Mawaziri wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
Mkurugenzi
Msaidizi Idara ya Biashara kutoka Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw.
Abdulla Makame Akiwaeleza waandishi wa Habari(hawapo pichani) Kuhusu Mkutano wa
29 wa Baraza la Mawaziri wa nchi
wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika Septemba 20 mwaka
huu Jijini Arusha. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara
hiyo Anthony Ishengoma.
Picha na Hassan Silayo
Frank
Mvungi- Maelezo
Mkutano
wa 29 wa Baraza la Mawaziri wa nchi
wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
utapokea na kuidhinisha aina mpya ya hati za kusafiria za kielektroniki,
zikiwemo sampuli za hati za kusafiria za kibalozi, za Maofisa na za kawaida.
Hayo
yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya
Biashara,Uwekezaji na shughuli za uzalishaji wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Dk. Abdulla Makame wakati wa
mkutano na waandishi wa habari.
Mkutano
huo utakaofanyika Septemba 20 mwaka huu Jijini Arusha pia unatarajia kupokea na
kuidhinisha taarifa mbalimbali sambamba na kutolea maamuzi masuala yanayohusu
mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Akieleza
zaidi Makame amesema mkutano huo utapokea na kuidhinisha aina mpya ya hati ya
kusafiria ya kielektroniki,zikiwemo sampuli za hati za kusafiria za kibalozi, za Maofisa na za kawaida za kusafiria.
Aidha
Mkutano huo utajadili mapendekezo na hadidu za rejea za uanzishwaji wa Dira ya
maendeleo ya Afrika Mashariki ya mwaka 2050.
Pia
mkutano huo utajadili mapendekezo ya mpango mwelekeo na shughuli mbalimbali
zinazolenga kuandaa katiba ya shirikisho la Afrika Mashariki na kujadili
mapendekezo ya baraza la ulinzi na usalama linalopendekezwa.
Baraza
la Mawaziri katika Jumuiya ya Afrika mashariki ni chombo cha pili katika ngazi
za kufanya maamuzi ndani ya Jumuiya ya
Afrika Mashariki baada ya Mkutano wa Kilele.
No comments:
Post a Comment