KUTUMIA MITANDAO YA KIJAMII SI DHAMBI, TUITUMIE VIZURI KWA MALENGO YALIYOKUSUDIWA.

Na Benedict Liwenga, Maelezo-DSM.
Mitandao ya kijamii ni mizuri katika
kuhabarisha umma endapo inatumiwa kulingana na madhumuni iliyotengenezwa, kwani
ina nguvu ya kusambaza habari kwa haraka na kwa wakati hapa duniani.
Pamoja na umuhimu nwa mitandao hii ya
kijamii, kuna baadhi ya watu ambao wao hujiona kuwa wameendelea katika
ulimwengu wa kisayansi na teknolojia kiasi cha kuanza kuitumia mitandao hiyo
kinyume na malengo kwa kutumia kuiba taarifa mbalimbali za watu na hata usalama
wa maeneo muhimu ikiwemo benki, ofisini, mashuleni na sehemu kadha wa kadha.
Watu hawa kwa jina la kisayansi na
teknolojia hujulikana kama ‘Hackers’ au Wezi wa mitandao kwa kisawahili, na
wamekuwa wakivumbua mbinu mbalimbali kila kukicha ili kuweza kutimiza adhma yao
ya kuingilia mitandao mingi iliyopo duniani na wakati mwimngine wamekuwa
wakitumika katika shughuli za kigaidi ulimwenguni.
Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali toka
mitandaoni, kuna mbinu nyingi zitumiwazo na hackers hawa katika kuiba taarifa
mbalimbali kutoka kwenye takirishi (Computer)
hata simu za mkononi kwa njia ya mtandao (internet)
na njia hizi huwa zimekuwa zikiboreshwa kila kukicha.
Wezi
wa mitandao wengi wamekuwa wakitumia visaidizi vya kompyuta (softwares)
zijulikanazo kama Keyloggers ambazo ni hatari sana katika
kuiba taarifa toka sehemu yoyote endapo tu mmiliki wa kompyuta ataiacha
kompyuta
yake kutumiwa na watu wasiofahamika ama katika ofisi mtu mharibifu
ataingia na
kuingiza katika mfumo wa kuongozea kompyuta kisaidizi kama hiko,
kutokana na
hilo software hizo hukusanya taarifa za mtu pasipo mtumiaji kujua
kinachoendelea na taarifa hizo hutumwa kwa njia ya barua pepe kwenda kwa
mharifu ambaye yeye anakuwa anazipata kadri atakavyo juu ya chochote
akifanyacho mtu, na moja ya sifa za software hizo ni kwamba hazionekani
ndani
ya mfumo wa kuongozea kompyuta kirahisi.
Mbinu nyingine watumiazo watu hao ni kwa njia ijulikanayo
kwa kimombo kama ‘Phising’ ambapo
ukurasa unaofanana sawia na ukurasa halisi wa website hutengenezwa kwa
madhumuni thabiti ya kuiba nenosiri ama taarifa zozote kuhusiana na kitu
chochote, njia hii ni hatari pia ingawa haina tofauti sana na njia ile ya key logging kwani katika njia hii kazi
kubwa inayofanyika ni kuweko kwa kurasa feki ambayo inayofanana na kurasa
halisi ya website fulani.
Ili tuweze kujikinga na matukio haya ya wizi wa taarifa
kwa njia ya mtandao kuna mambo muhimu ya kuzingatia ambayo tunapaswa kuwanayo
makini wakati wote tunapozitumia kompyuta zetu.
No comments:
Post a Comment