BILL GATES AIPIGA TAFU AFRIKA MAGHARIBI KWA KUCHANGIA DOLA MILIONI 50 KUPAMBANA NA EBOLA
Tajiri nambari moja Duniani na muanzilishi wa kampuni ya Microsoft, Bill Gates na mkewe Melinda kupitia mfuko wao wa The Bill & Melinda Gates Foundation
wamejitolea kuipiga tafu Afrika Magharibi kwa kuchangia kiasi cha dola
za kimarekani milioni 50 ambazo ni sawa na bilioni 80 za kitanzania
katika kupiga vita ugonjwa hatari wa Ebola.
Bill Gates na mkewe walitangaza jumatano iliyopita kupitia
mtandao wa Twitter kuchangia kiasi hicho kikubwa cha pesa kwa ajili ya
kuutokomeza ugonjwa huo hatari ulioshika kasi kwa nchi za Afrika
Magharibi.
Habari zinaeleza kwamba kiasi hicho cha hela kinatajwa kuwa
ni kikubwa kuwahi kuchangiwa na mifuko ya watu binafsi ambapo awali
mfuko huo ulikuwa tayari umeshachangia kiasi cha dola za kimarekani
milioni 10.
”Kwa kupambana na Ebola sasa, tunaweza kuhakikisha halitakuwa janga katika Afrika Magharibi”, aliandika Bill Gates kwenye ukurasa wake wa Twitter
Rekodi hiyo inakuja kufuatia maombi yaliyotolewa na katibu
mkuu wa umoja wa mataifa Bwana Ban Ki-Moon ya dola milioni 600 kwa ajili
ya kupambana na janga hilo ambalo mpaka sasa limeshauwa watu takribani
2000 kutoka Liberia, Nigeria, na Sierra Leone.
Taarifa kutoka Gates Foundation ilisema: ”Hadi
sasa, the Gates Foundation ina nia ya kujitolea zaidi ya dola milioni 10
kati ya dola milioni 50 kupambana na Ebola, ikiwa ni pamoja na dola
milioni 5 kwa shirika la afya Duniani(WHO) kwa ajili ya shughuli za
dharura na tathimini na dola milioni 5 kwa mfuko wa Marekani kwa ajili
ya UNICEF kuunga mkono juhudi katika kuisaidia Liberia, Sierra Leone na
Guinea kununua mahitaji muhimu ya matibabu, kuratibu shughuli za majibu
na kuitoa katika hatari jamii na habari za afya”.
Alhamisi ya Septemba 11, Reuters iliripoti kuwa mwanzilishi
mwenza wa kampuni ya Microsoft, Paul Allen alikuwa atangaze kwamba
angetoa dola milioni 9 kwa kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa kwa
ajili ya kusaidia kupambana na virusi hivyo.
Chanzo : Business Insider
No comments:
Post a Comment