NMB YAWAKOMBOA VIJANA KIUCHUMI KWA KUWAPA MIKOPO NAFUU YA PIKIPIKI
·
Ni mikopo kwa ajili ya
pikipiki za miguu miwili na mitatu
Benki ya
NMB kwa kushirikiana na kampuni tatu yaani Fair Deal Auto Private Ltd inayosambaza pikipiki za miguu miwili na mitatu aina
ya Bajaji, kampuni ya Car & General Limited Ltd inayosambaza pikipiki za
miguu mitatu aina ya TV’S King pamoja na kampuni ya Quality Motors inayosambaza
pikipiki za miguu miwili aina ya Honda wameingia ubia ili kuwawezesha wananchi
kupata mikopo nafuu ya kumiliki pikipiki za miguu miwili na mitatu.
Hii yote ni katika kuendeleza azma ya NMB inayolenga kubuni
huduma na bidhaa mbali mbali za kibenki zinazogusa kwa karibu mahitaji ya wateja
na watanzania kwa ujumla.
Waziri
wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu uwekezaji na uwezeshwaji, Mhe. Dkt Mary Nagu akikata
utepe kama ishara ya ufunguzi rasmi wa uwezeshwaji kwa wateja wa NMB kupitia
mikopo ya pikipiki za miguu miwili na mitatu kutoka benki ya NMB.
Uzinduzi huo ulifanyika katika hoteli ya Tilapia ya jijini Mwanza
Akizungumza
katika hafla ya uzinduzi wa mikopo hii jijini Mwanza, Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji kutoka
ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Dkt. Mary Nagu amesema “Mikopo hii ya pikipiki itawasaidia sana
vijana na wananchi kwa ujumla kuweza kumiliki pikipiki zitakazowawezesha
kuendesha maisha yao ya kila siku. Binafsi natambua ajira kwa vijana imekua ni
changamoto maeneo mengi nchini hivyo basi ningependa kuwasisitiza vijana
wachukue fursa hii inayotolewa na NMB kuweza kumiliki biashara zao wenyewe na
kujikimu kiuchumi.”
Waziri wa nchi ofisi ya Waziri
Mkuu uwekezaji na uwezeshwaji, Mhe. Dkt. Mary Nagu akipeana mkono na Mkuu wa
Mkoa wa Geita Saidi Magalula wakati wa uzinduzi huo.
Vilevile kutoka NMB, Mkuu wa Kitengo cha Biashara za kibenki,
Bw. Filbert Mponzi amesema kuwa bidhaa hii mpya ina lenga kupunguza
changamoto za ajira kwa vijana hapa nchini.
“NMB itaendelea kubuni bidhaa
ili kupambana na changamoto za ajira zinazowakumba wateja. tutaendelea
kushirikiana na makampuni kama Fair Deal Auto Private Ltd, Car & General Limited Ltd pamoja na
Quality Motors ili kupata bidhaa zenye ubora zaidi.” alisema Mponzi.
Waziri wa nchi ofisi ya Waziri
Mkuu uwekezaji na uwezeshwaji, Mhe. Dkt. Mary Nagu akimpongeza Mkuu wa Kitengo
cha Biashara za benki ya NMB, Bw. Filbert Mponzi wakati wa uzinduzi wa mpango
wa uwezeshwaji kwa wateja wa NMB kupitia mikopo ya pikipiki za miguu miwili na
mitatu kutoka benki ya NMB. Kushoto ni Meneja wa NMB Kanda ya ziwa, Bw.
Straton Chilongola.
Marejesho ya mkopo huu wa pikipiki ya miguu
miwili na mitatu yanatolewa ndani ya muda wa miezi 24, ambapo kwa kipindi hiki chote,
mteja ataendelea kurejesha makato yake ya kila mwezi kwa kuzingatia taratibu za
makubaliano yatakayofanyika baina ya mteja na benki ya NMB.
Mikopo hii pia inawekewa bima kwa ajili ya
ulemavu au kifo kitakachomtokea mmliki wa pikipiki iliyochukuliwa mkopo. Bima
hii ni kwa ajili ya kumpa unafuu mkopaji endapo atapata matatizo ya kiafya
ambayo yatamfanya apate ulemavu au kupoteza maisha.
Mikopo hii yenye masharti nafuu inatolewa kwa mteja yeyote ambaye
atatitimiza vigezo vilivyowekwa ili kupata mkopo huu. Anachotakiwa kufanya
mteja ni kulipia asilimia thelathini ( 30%) ya bei ya pikipiki ya miguu miwili au mitatu kama inavyouzwa na wasambazaji wa pikipiki
hizi za Fair Deal Auto Private Ltd , Car & General Ltd pamoja na Quality
Motors.
Kwa maelezo zaidi temembelea matawi ishirini na moja tu ya NMB nchi
nzima yanayotoa mikopo hii kama ifuatavyo:
Mwanza -Buzuruga na Kenyata Road,
Dar es Salaam-Tegeta, Magomeni, Mwenge, Mbezi Beach,
Temeke, Ilala, Mlimani City, Msasani na Airport
Arusha-Clock Tower na Arusha Market
Manyara-Babati na Katesh
Dodoma
Mbeya-Mwanjelwa, Mbalizi Road na Usongwe
Moshi-Nelson Mandela na Tanga-Madaraka
NMB BENKI YAKO



No comments:
Post a Comment