*CHONDE CHONDE WATANZANIA TUJITOE KUOKOA MAISHA YA MTOTO HANIFAH
Mtoto Hanifa, akiwa amelazwa hospitali akipatiwa matibabu.
Mtoto Hanifa, akiwa amelazwa hospitali akipatiwa matibabu.
Mtoto
Hanifa Salum Hassan mwenye umri wa miaka mitano anasumbuliwa na ugonjwa
wa Saratani ya Damu (Leukemia) ambao umemfanya ashindwe kusimama na
kutembea, anasumbuliwa na maumivu ya kichwa wakati wote, wakati mwingine
hushindwa kupumua hivyo kulazimika kupumua kwa kutumia mashine pia
hawezi kula analishwa kwa kutumia mirija na pia kila baada ya muda
inabidi abadilishiwe damu.
MATIBABU
Matibabu
ya mtoto Hanifa ni ya gharama kubwa sana. Ugonjwa wake haukujulikana
alipopelekwa Hospitali ya taifa Muhimbili lakini alipopelekwa nchini
India gharama za uchunguzi pekee zilikuwa dola 7,600 ambapo mtoto Hanifa
aligundulika kuwa na ugonjwa wa Acute lymphoblastic Leukemia. Matibabu
yake yalipangwa yawe kwa awamu tatu ambapo awamu ya kwanza ya matibabu
iligharimu dola 10,000.
Mwisho
wa awamu ya kwanza zilihitajika dola 10,000 zingine ili aingie kwenye
awamu ya pili ya matibabu lakini uwezo wa ndugu na jamaa ulikuwa ndio
umeishia hapo hivyo matibabu ya mtoto Hanifa yalilazimika kukatishwa na
Hanifa kurudishwa Tanzania. Ripoti za madaktari India zilipelekwa
Muhimbili ambapo matibabu ya mtoto Hanifa yalipangwa kugharimu Tsh.
milioni 2 kwa mwezi.
Hakuna
pesa za kumwezesha mtoto kuanza matibabu Muhimbili hivyo mtoto Hanifa
amebaki nyumbani jijini Dar es Salaam akiwa kwenye hatari kubwa ya
maambukizi mbalimbali ambayo yanaweza kuhatarisha maisha yake.
Hadi
sasa ndugu na jamaa wanahaha kutafuta pesa za kumwezesha mtoto Hanifa
kumalizia awamu mbili za matibabu yake nchini India kama ikiwezekana au
ikishindikana basi aweze kuanza matibabu Muhimbili.
MICHANGO
Kwa watakaopenda kujitolea kuokoa maisha ya Mtoto Hanifa wanaombwa watoe michango yao kupitia akaunti hizi
Kwa walio Tanzania
Jokha Khamis Issa
Akaunti Namba: 041212000428
People Bank of Zanzibar
Kwa walio nje ya Tanzania wanaweza kutuma michango yao kwa akaunti hii
Suleiman Maadini
Account Number: 15092968
Sort Code: 30-67-99
Bank: Lloyds TSB
Country: United Kingdom



No comments:
Post a Comment