KATIBU MKUU KIONGOZI BALOZI OMBENI SEFUE ATEMBELEA OFISI ZA WAKALA YA SERIKALI MTANDAO LEO JIJINI DAR ES SALAAM.
. Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiongea na viongozi wa Wakala
ya Serikali Mtandao na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam
mara baada ya kupokea taarifa kuhusu maendeleo ya Tovuti Kuu mpya ya
serikali inayosimamiwa na Wakala ya Serikali Mtandao chini ya Ofisi ya
Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma. Balozi Sefue amefafanua kuwa Tovuti
Kuu ya Serikali iliyoanzishwa itawawezesha wananchi kupata taarifa na
huduma mbalimbali zinazotolewa na serikali.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Dkt. Jabiri Bakari akiongea na
waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu mpango wa serikali
katika kuhamasisha na kuendeleza matumizi
ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika shughuli za serikali
kupitia Tovuti Kuu mpya ya serikali iliyoanzishwa kwa lengo la
kuboresha na kurahisisha utoaji wa taarifa na huduma kwa umma,
kuhamasisha ushirikishwaji wa raia katika utoaji wa maamuzi yanayowahusu
na kuwezesha uwepo wa serikali iliyo wazi.
Baadhi
ya viongozi wa Wakala ya Serikali Mtandao iliyo chini ya Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na waandishi wa habari wakiwa katika
mkutano na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.
Mwonekano mpya wa Tovuti Kuu ya Serikali ambayo inapatikana katika anuani ya www.egov.go.tz
Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (katikati) akiwasili katika ofisi za
Wakala ya Serikali Mtandao zilizopo jengo la TTCL mtaa wa Samora leo
jijini Dar es salaam kwa lengo la kuangalia shughuli za usimamizi wa
mifumo na matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
katika uendeshaji wa shughuli za serikali.
No comments:
Post a Comment